Baadhi ya wajane wakiwa katika maandamano ya kusheherekea Siku ya wajane Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenzwa na wajane wakati alipotembekea banda la Mtandao wa wajane Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia bidhaa za vikombe zinazotengenzwa na kikundi cha Maasai Market kutoka Kanda ya Kaskazini wakati alipotembekea banda lao katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wajane na wagane katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yalioyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu akielezea historia ya Siku ya Wajane Duniani wakati wa Maadhimisho ya Siku hiyo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa cheti kwa mwakilishi wa wajane Kanda ya Ziwa Bi. Rehema Said kwa kuwa moja ya mabanda matatu bora katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea bango lenye kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wajane Dunaiani kutoka kwa Mtandao wa Wajane Tanzania (TAWIA) katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wajane wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa aktika picha ya pamoja na wawakilishi wa wajane kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani katika maadhimisho ya Siku ya Wajane yaliyofanyika jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
……………..
Na Mwandishi Wetu- Dodoma.
Naibu Waziri wa Afyaya, Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa Wizara yake na TAMISEMI kutoa elimu kwa Jamii hususani kuhusu mirathi na uandishi wa wosia ili jamii iweze kutambua umuhimu wa mirathi na wosia na kuondokana na migogoro mingi inayowakumba wajane Nchini.
Naibu Waziri Ndugulile ameyasema hayo leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani yaliyofanyika Kitaifa leo Jijini Dodoma na kusisitiza kuwa elimu ya mirathi na uandishi wa wosia ni muhimu kwa sababu idadi kubwa ya watu bado haijui haki zake.
Aidha Dkt. Ndugulile amewataka wanandoa kote Nchini kuhakikisha wanasajili ndoa zao ili wajane na watoto waweze kupata haki zao lakini pia akawataka wananchi kuiga mfano wa Nchi za Ulaya ambapo kabla ya kufunga ndoa kila mmoja utaja mali zake ili zisiwe sehemu ya mirathi inapotokea kuna kufarakana au mmoja kufariki.
Dkt. Ndugulile ameonya kuwa maandalizi ya mirathi na wosia yaanze sasa bila kusubiri vifo na kuwataka watu kufahamu kuwa mtu kuwa mjane sio mwisho wa maisha bali watambue kuwa mwenzako anapoondoka maisha yanapaswa kusonga mbele.
Aidha Naibu Waziri Ndugulile amewataka wadau wote Nchini kukutana na Wizara yake ili kupitia Sera ya Taifa ya maendeleo ya Wanawake na Jinsia na kuahakikisha masuala yote ya mirathi na ukatili wa kijinsia yanazingatiwa kulingana na wakati huo akiwataka wasanii kutumia sanaa yao kuelimisha umma kuhusu madhira na madhara yawakutayo wajane hao.
Aidha Mgane wa Kiume Bw. Eliona Makundi akitoa ushuhuda wake kwa wanaume wafiwa ameonya wanaume kutokimbilia kuoa bali watunze watoto wao mpaka wafikie ndoto zao kwani ukikosa umakini mwanamke wa kambo anaweza akasababisha familia kusambaratika.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa maadhimisho haya yanafanyika Jijini Dodoma kwa mara ya kwanza Kitaifa na yamewakutanisha Wajane wote kutoka mikoa 20 ya Tanzania bara na Wizara yake imewapatia fursa ya kuwajengea uwezo wajane hao kuhusu ujasiliamali na stadi mbalimbali za maisha.
Katibu Mkuu Jingu ameongeza kuwa azimio la kuitambua tarehe 23 Juni kuwa Siku ya Wajane Duniani ni kutokana na Changamoto mbalimbali ikiwemo umasikini, unyanyapaa na kudhulumiwa haki zao za msingi za kijamii na kiuchumi na kuongeza kuwa dunia kwa sasa ina zaidi ya wajane 258 milioni na mmoja kati ya Wajane 10 wanaishi katika umasikini wa kutupwa.
Maadhimisho haya yanafanyika Duniani kote kwa lengo la kutoa Msukomo kwa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za makusudi kutokomeza umasikini na uonevu unaowakabili wajane kote Duniani.