Home Mchanganyiko IGP SIRRO ASHIRIKI MASHINDANO YA MBIO ZA DASANI MARATHON

IGP SIRRO ASHIRIKI MASHINDANO YA MBIO ZA DASANI MARATHON

0

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kushoto), akitoa ishara ya kuanza
kwa mashindano ya mbio za Dasani Marathon, zilizofanyika leo 23/06/2019
jijini Dar es salaam, ambapo wakimbiaji walikimbia umbali wa Kilomita 21,
Kilomita 10 na Kilimita 05, IGP Sirro ni miongoni mwa washiriki wa mbio za
kilomita 10. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (Wapili kushoto), akishiriki
mashindano ya mbio za Dasani Marathon Kilomita 10, zilizofanyika leo jijini
Dar es salaam, ambapo washindi kwenye mashindano hayo walijinyakulia
zawadi mbalimbali walizokabidhiwa na mgeni rasmi IGP Sirro Sirro. Picha
na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akikabidhi zawadi kwa Natalia
Elisante mshindi wa mbio za Dasani Marathon kilomita 21 kwa upande wa
wanawake zilizofanyika leo 23/06/2019 jijini Dar es salaam, IGP Sirro
alikuwa mgeni rasmi kwenye mashindano hayo. Picha na Jeshi la Polisi.

Washindi wa mbio za Dasani Marathon kilomita 21 kwa upande wa
wanaume wakionyesha mfano wa hundi walizokabidhiwa na Mgeni rasmi
kwenye mashindano hayo ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon
Sirro (hayupo Pichani) zilizofanyika leo jijini Dar es salaam, IGP Sirro naye
ni miongoni mwa walioshiriki mbio za kilomita 10. Picha na Jeshi la Polisi.