…………………….
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Mb) amesema ujenzi unaoendelea wa shule ya mfano inayojengwa Mkoani Dodoma haiendani na viwango vya mfano ambavyo mtu yeyote akija atatambua kuwa hiyo ndio shule ya mfano.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo ya Msingi inayojengwa katika Kata ya Ipagala Jijini Dodoma wakati wa ziara yake Waziri Jafo ameyasema alitegemea kukuta kitu kitofauti na alichokikuta eneo la ujenzi kwa sababu Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.
“Ujue mpaka shule inapewa hadhi ya kuwa ya mfano inatakiwa iwe ya utofauti mkubwa sana na shule za kawaida kuanzia kwenye ramani ya majengo, ukubwa wa eneo, muonekano wa majengo yanayojengwa, mandhari, viwanja vya michezo na kila kitu kitakachowekwa katika shule hiyo” Amesema Jafo
Aliongeza kuwa Sasa kwa hapa Ipagala kwanza ukiingia tu unaanza kuona eneo la shule limezingirwa na makazi ya watu kwa karibu sana halafu majengo yanayojengwa yote ni ya chini kama mabehewa ya Treni hamuoni kwa eneo lililopo hapa hamtapata nafasi ya kutosha kwa ajili ya kufanya vitu vingine vya Msingi.
Aidha Mhe. Jafo alifafanua kuwa “eneo mlilonalo la Ekari saba sio dogo kwa ujenzi wa shule ya kawaida lakini sio lakini kubwa kwa ujenzi wa shule ya mfano yaan hapa mlitakiwe mpate ekari hata thelathini kuwe na nafasi ya kutosha kisha mjenge majengo ya gorofa, vipatikane viwanja vya michezo vizuri, maeneo ya kupumzikia watoto na nyumba za walimu ziwe pembeni kidogo sio vitu vyote visongamane katika eneo moja;
Hii ni shule ya mfano inatakiwa kuwa na muonekano ambao kila mtu akija hapa atakubali kuwa kweli hapa ni eneo la mfano na wengine watakuja kujifunza kwaiyo sitafurahia kuona vitu vya kawaida kawaida tu lazima mjue kujiongeza”.
Aliongeza kuwa sitegemei kuona shule hii inafanana na shule ya Msingi Chaduru au Nzuguni B lazima iwe tofauti katika kila kitu, mkifanya mchezo nyie Dodoma ndio mtakuwa tofauti na wenzenu wote wanaojenga shule hizi za Mfano na watawazidi endeleni kufikiria kawaida tu.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Belnith Mahenge alikiri kuwa wataalamu wa Dodoma hawakupanua mawazo yao katika kuangalia namna bora ya kutekeleza ujenzi wa shule ya mfano katika Mkoa wa Dodoma.
“Nikiri tu kuwa tumekosea na baada ya ziara hii ya Mhe. Waziri tukaa pamoja na wataalamu wetu kuangalia namna gani tunaweza kurekebisha kasoro hizi zilizojitokeza katika ujenzi huu wa Shule ya Mfano ili iwe na ubora unatakiwa katika shule hizi” Alisema Mahenge.
Naye Mkurgenzi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Julius Nestory ametaja vigezo vya shule za Mfano kuwa ni Uwepo wa Vyumba vya madarasa kuanzia 17 tofauti na shule za kawaida ambazo zina vyumba sita mpaka tisa na shule hiyo itajengwa eneo lenye idadi kubwa ya watu ambapo pia kutakua na idadi kubwa ya wanafunzi.
Nestory aliendelea kutaja vigezo vya shule ya mfano kuwa ni uwepo wa miundombinu muhimu kama Nyumba za Walimu, Maktaba, Ukumbi wa Mikutano, Jengo la Utawala, vyoo vya kutosha pamoja na viwanja vya michezo.
Alimaliza kutaja maeneo ambayo shule hizo zitajengwa Nchini kuwa ni Dodoma eneo la Ipagala, Kigome kule Buhigwe, Geita, Mtwara katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na Mara kwenye shule aliyosoma Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere ambayo ni Shule ya Msingi Mwisenge.
Naye Afisa Elimu Msingi Jiji la Dodoma Joseph Mabeyo amesema walipokea Tsh Mil 706 mnamo mwezi April 2019 na ujenzi unaondelea utahusisha vyumba vya madarasa 17, Maktaba, Bwalo la chakula, nyumba za walimu, matundu ya vyoo pamoja na Jjengo la Utawala na ujenzi huo unategemea kukamilika Mwezi Agosti, 2019.
…………………….Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMIWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Mb) amesema ujenzi unaoendelea wa shule ya mfano inayojengwa Mkoani Dodoma haiendani na viwango vya mfano ambavyo mtu yeyote akija atatambua kuwa hiyo ndio shule ya mfano.Akikagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo ya Msingi inayojengwa katika Kata ya Ipagala Jijini Dodoma wakati wa ziara yake Waziri Jafo ameyasema alitegemea kukuta kitu kitofauti na alichokikuta eneo la ujenzi kwa sababu Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.“Ujue mpaka shule inapewa hadhi ya kuwa ya mfano inatakiwa iwe ya utofauti mkubwa sana na shule za kawaida kuanzia kwenye ramani ya majengo, ukubwa wa eneo, muonekano wa majengo yanayojengwa, mandhari, viwanja vya michezo na kila kitu kitakachowekwa katika shule hiyo” Amesema JafoAliongeza kuwa Sasa kwa hapa Ipagala kwanza ukiingia tu unaanza kuona eneo la shule limezingirwa na makazi ya watu kwa karibu sana halafu majengo yanayojengwa yote ni ya chini kama mabehewa ya Treni hamuoni kwa eneo lililopo hapa hamtapata nafasi ya kutosha kwa ajili ya kufanya vitu vingine vya Msingi.Aidha Mhe. Jafo alifafanua kuwa “eneo mlilonalo la Ekari saba sio dogo kwa ujenzi wa shule ya kawaida lakini sio lakini kubwa kwa ujenzi wa shule ya mfano yaan hapa mlitakiwe mpate ekari hata thelathini kuwe na nafasi ya kutosha kisha mjenge majengo ya gorofa, vipatikane viwanja vya michezo vizuri, maeneo ya kupumzikia watoto na nyumba za walimu ziwe pembeni kidogo sio vitu vyote visongamane katika eneo moja;Hii ni shule ya mfano inatakiwa kuwa na muonekano ambao kila mtu akija hapa atakubali kuwa kweli hapa ni eneo la mfano na wengine watakuja kujifunza kwaiyo sitafurahia kuona vitu vya kawaida kawaida tu lazima mjue kujiongeza”.Aliongeza kuwa sitegemei kuona shule hii inafanana na shule ya Msingi Chaduru au Nzuguni B lazima iwe tofauti katika kila kitu, mkifanya mchezo nyie Dodoma ndio mtakuwa tofauti na wenzenu wote wanaojenga shule hizi za Mfano na watawazidi endeleni kufikiria kawaida tu.Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Belnith Mahenge alikiri kuwa wataalamu wa Dodoma hawakupanua mawazo yao katika kuangalia namna bora ya kutekeleza ujenzi wa shule ya mfano katika Mkoa wa Dodoma.“Nikiri tu kuwa tumekosea na baada ya ziara hii ya Mhe. Waziri tukaa pamoja na wataalamu wetu kuangalia namna gani tunaweza kurekebisha kasoro hizi zilizojitokeza katika ujenzi huu wa Shule ya Mfano ili iwe na ubora unatakiwa katika shule hizi” Alisema Mahenge.Naye Mkurgenzi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Julius Nestory ametaja vigezo vya shule za Mfano kuwa ni Uwepo wa Vyumba vya madarasa kuanzia 17 tofauti na shule za kawaida ambazo zina vyumba sita mpaka tisa na shule hiyo itajengwa eneo lenye idadi kubwa ya watu ambapo pia kutakua na idadi kubwa ya wanafunzi.Nestory aliendelea kutaja vigezo vya shule ya mfano kuwa ni uwepo wa miundombinu muhimu kama Nyumba za Walimu, Maktaba, Ukumbi wa Mikutano, Jengo la Utawala, vyoo vya kutosha pamoja na viwanja vya michezo.Alimaliza kutaja maeneo ambayo shule hizo zitajengwa Nchini kuwa ni Dodoma eneo la Ipagala, Kigome kule Buhigwe, Geita, Mtwara katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na Mara kwenye shule aliyosoma Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere ambayo ni Shule ya Msingi Mwisenge.Naye Afisa Elimu Msingi Jiji la Dodoma Joseph Mabeyo amesema walipokea Tsh Mil 706 mnamo mwezi April 2019 na ujenzi unaondelea utahusisha vyumba vya madarasa 17, Maktaba, Bwalo la chakula, nyumba za walimu, matundu ya vyoo pamoja na Jjengo la Utawala na ujenzi huo unategemea kukamilika Mwezi Agosti, 2019.