NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
K-VIS BLOG/Khalfan Said
BODI
ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), pamoja na Menejimenti ya Mamlaka
hiyo, zimemefanya ziara kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
ili kujionea jengo jipya la kiwanja hicho, Terminal
III (TBIII), pamoja na Maktaba mpya na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam sehemu ya Mlimani.

Ziara
hiyo iliyofanyika Ijumaa Juni 21, 2019 pia iliwahusisha wajumbe wa Kamati ya
Maudhui ya TCRA.
hiyo iliyofanyika Ijumaa Juni 21, 2019 pia iliwahusisha wajumbe wa Kamati ya
Maudhui ya TCRA.
Akizungumzia nia ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba
alisema, Mamlaka kama Mdhibiti na Msimamizi wa Mawasiliano nchini, imeona ni
vema kutembelea taasisi hizo mbili kwani kuna mambo ya msingi yanayofanywa na
taassi hizo yanahusiana moja kwa moja na huduma zinazotolewa na TCRA.

“Lengo
la ujio wetu hapa Terminal III nikuangalia katika hatua hizi ambazo ujenzi
umekamilika ni mahitaji yapi ambayo bado ili sisi tuongeze ushiriki wetu ili
kuyakamilisha hususan katika mifumo ya mawasiliano.” Alsiema Mhandisi Kilaba.

Alisema wakiwa hapo TBIII wamepata fursa ya kuulizia hali ya mawasiliano kama imekamilika ambapo watoa huduma, TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo, Zantel, Halotel na hata Internet kama wako tayari.
“Huduma
hizi ni muhimu sana na zinatakiwa ziwe kwenye maeneo kama haya kwa sababu
zinawezesha hata kufanya utalii kuwa rahisi, mgei anapoingia hapa na anataka kwenda
eneo Fulani la utalii lazima awasiliane, lakini pia TCRA inatoa masafa kwa
ajili ya kuongozea ndege zinapotua na kuruka na lengo hasa ni kuhakikisha
hakuna muingiliano katika huduma hizo.” Alibainisha Mkurugenzi huyo Mkuu wa TCRA.

“Kuja kwetu kumetupa fursa ya kujifunza mengi kama
ambavyo watanzania wanaweza kushuhudia kuwa kiwanja hiki ni kizuri, kinapendeza na
mawasiliano yapo yanaendelea kukamilishwa na tumejionea hata Wifi point ipo.”
Alifafanua Mhandisi Kilaba.
ambavyo watanzania wanaweza kushuhudia kuwa kiwanja hiki ni kizuri, kinapendeza na
mawasiliano yapo yanaendelea kukamilishwa na tumejionea hata Wifi point ipo.”
Alifafanua Mhandisi Kilaba.
Aidha
kuhusu Maktaba mya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhandisi Kilaba
alisema, Maktaba hiyo inatumia huduma za TCRA kwani moja ya huduma zitolewazo ni
pamoja na Maktaba mtandao (e-library) na hili ni jambo jema.

Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt.Jones Killimbe alisema, ziara hiyo
imekuwa ni ya mafanikio makubwa kwani imewezesha timu nzima ya TCRA, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti, Wajumbe wa Kamati zinazosaidia kutekeleza majukumu kwenye
mamlaka kwa pamoja wameelimika sana.

“Kiwanja
hiki katika lugha ambayo ningeiazima ni flagship
project….ni mradi wa kimkakati wa taifa hili… nikisema kimkakati ni kwasababu
mojawapo ya masuala ya kiuchumi ya nchi yetu ni utalii, na nadhani huu utakuwa
mlango mkubwa sio dirisha…utakuwa mlango mkubwa wa utalii na mchango wa utalii
kwenye uchumi wetu utaongezeka sana.” Alisema Dkt. Killimbe.

hiyo imewezesha wajumbe kupata maelezo ya kina ya kukamilika kwa huduma mbalimbali kwenye jengo la TBIII hali kadhalika kwenye maktaba ya ksiasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa,
hiyo imewezesha wajumbe kupata maelezo ya kina ya kukamilika kwa huduma mbalimbali kwenye jengo la TBIII hali kadhalika kwenye maktaba ya ksiasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa,
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (mwenye shati jeupe), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba, (kulia), wajumbe wa Bodi na Kamati ya Maudhui ya TCRA wakiongozwa na Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa jingo la Terminal 3 (TBIII) la kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Juni 21, 2019.
Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mhandisi Kilaba, wakitembelea eneo la kusubiri abiria la jingo la TBIII kabla ya kuingia ndani ya ndege.
Muonekano wa nje wa eneo la kuondokea abiria kwenye jingo jipya la TBIII la kiwanja cha ndege cha Julkius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ujumbe wa TCRA ukipatiwa maelezo na Mhandisi Barton Komba (kulia), kuhusu wapi abiria anapaswa kuelekea mara tu baada ya kuingia eneo la kuondokea abiria.
Mandhari ya sehemu ambayo abiria wa kawaida watakuwa wakisubiri kabla ya kupanda ndege.
Eneo la udhibiti wa Pasipoti mara tu baada ya abiria kuwasili kwenye kiwanja hicho.
Mhandisi Komba (kushoto), akimpitisha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA eneo litakalotumika kudhibiti pasipoti.
Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Bw. Jacob Tesha, akizunhumza jambo ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya huduma kwenye jingo hilo.
Eneo la ku chek-inn.
Picha ya pamoja.
Msimamizi wa Maktaba mpya na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (eneo la nyaraka za serikali), akitoa maelezo kwa ujumbe wa TCRA ukiongozwa na Mwenyekiti wa bodi, Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (mwenye nguo za kibuluu), wakati wa ziara ya kutembelea maktaba hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, TCRA), Bi. Valerie Msoka (kushoto) na mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Bw. Dreck Murusuri, wakiangalia jinsi maktaba ya kielektroniki (e-library)ya Maktaba ya kisasa ya UDSM inavyofanya kazi.
Mkurugenzi Mkuu, TCRA, Mhandisi James M. Killaba (wapili kulia), akiangalia kwa makini jinsi maktaba ya kielektroniki (e-library) ya Maktaba ya kisasa ya UDSM inavyofanya kazi.
Mwenyekiti wa bodi, Dkt. Jones Killimbe (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James M. Kilaba (mwenye nguo za kibuluu), pamoja na ujumbe wakiouongoza, wakiwa kwenye chumba cha maktaba ya kielektroniki (e-library) ya Maktaba hiyo ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maktaba mpya ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt.Esther Ndenje Sichalwe (katikati), akiongoza ujumbe wa TCRA ulipotembelea maktaba hiyo Juni 21, 2019.
Dkt. Sichalwe (kulia), akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitenmgo cha Mawasilian, Uhusiano na Elimu kwa Umma, TCRA, Bw. Semu Mewakyanjala, wakati wa ziara hiyo.
Picha ya pamoja ya ujumbe wa TCRA mara baada ya kutembelea maktaba hiyo.