Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozana na wataalamu kutoka Kikosi cha Uzalishaji cha Jeshi la Polisi na Wasimamizi wa Mradi kutembelea eneo la Kunduchi ambako Mradi wa Nyumba Mia Tatu Thelathini za Makazi ya Polisi zinazoonekana pichani zikiwa zishakamilika.Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, akimuelekeza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kutembelea eneo la Mikocheni ambako kumejengwa nyumba zinazoonekana pichani ikiwa ni makazi kwa ajili ya askari polisi. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, akitoa taarifa ya hali ya uhalifu katika mkoa wake kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati naibu waziri alipofika kituo cha polisi Oysterbay. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo Kipya cha Polisi Oysterbay. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi