Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal, +255756413465
Katika swala la kujifunza katika
jamii yetu bado limekuwa ni gumu sana. Ukikutana na watu kumi ukiwauliza
unapenda kusoma vitabu utasikia wakisema napenda kusoma vitabu ila sina muda.
Muda umekuwa kisingizio kwa watu wengi kutupia lawama zao zote katika muda.
Watu wanasingizia muda umekuwa tatizo lakini mimi nakataa nasema muda sio
tatizo. Habari njema ni kwamba Mungu ametuzawadia zawadi au rasilimali muhimu
kuliko zote ambayo ni muda. Kila binadamu aliye hai ana muda wa masaa 24 kwa
siku hivyo kwa wiki moja kila mtu ana jumla ya masaa 168 sasa katika masaa 168
kwa wiki nzima unakosa muda kweli wakusoma vitabu na kuongeza maarifa?

Ni hivi karibuni tu wakati wa ziara
ya Kikazi katika Wilaya ya Itilima vilevile Wilaya ya Bariadi, Waziri wa Kilimo
alizuru kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa biashara ya Pamba ili kumulika
madhila wanayopata wananchi kwa kucheleweshewa fedha kutokana na sintofahamu ya
wanunuzi kujitokeza kwa wingi katika ununuzi pamoja na wakulima kuwa tayari
wamekusanya Pamba kupitia vyama vyao vya Ushirika. Hapa Mhe Japhet Hasunga anakutana
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka huku akiwa na vitabu zaidi ya 100
ofisini kwake alivyokwishavisoma katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kama mchambuzi na mdadisi wa mambo
nilifanya mazungumzo ya takribani dakika 15 hivi kubaini dhana ya kusoma
vitabu, Uongozi na Uwajibikaji. Rc Mtaka anasema “Comrade Mathias akili yako
inahitaji maarifa kila siku ili iweze kukua, akili yako inahitaji chakula kila
siku kama unavyolisha tumbo lako nalo linahitaji maarifa. Hazina ya akili yako
ni maarifa na maarifa yanapatikana katika kusoma vitabu, makala chanya, na siyo
kusoma magazeti ya udaku, kusikiliza habari nyepesi nyepesi zisizokuwa na
upembuzi yakinifu.

Jinsi unavyokaa bila kusoma ndivyo akili yako inakaa inazidi
kulala ukisoma nayo inazidi kuamka. Jitahidi kusoma na kufikiri kila siku ndio
zoezi la akili yako. Kuwa na shahada, astashahada, stashahada, uzamili na
uzamivu siyo mwisho wa kusoma au kujifunza bali huo ndio mwanzo wa kujifunza.
Usiridhike na maarifa uliyonayo bali kuwa na njaa kali ya maarifa elimu
uliyopata darasani ni msingi tu wa kusoma. Mtu anayesoma anakuwa tofauti sana
na mtu asiyesoma vitabu tafadhali nakuomba anza kujifunza kuna faida nyingi
zisizoelezeka.

Kusoma vitabu sio jambo la lelemama
ni jambo la kufanya maamuzi na kutenga muda maalumu kwa ajili hiyo, Lengo kubwa
linalowafanya waandishi wa vitabu kuandika vitabu ni kuweka maarifa yao kwenye
maandishi, Kwa hakika vitabu huongeza sana uwezo wa kufikiri. Unaposoma vitabu
unafahamu mambo ambayo yatakufanya ufikiri zaidi; mara nyingine kitabu
kitakuacha na maswali ambayo yatakufanya utafakari kwa kina zaidi juu ya mambo
mbalimbali.

Rc Mtaka ni kijana kabisa kiumri
ambaye hajavuka hata miaka 40 bila shaka. Anaeleza Maisha yana changamoto
mbalimbali; hivyo utahitaji kitu cha kukuhamasisha kutoka hatua moja hadi
nyingine. Kwa kusoma vitabu vya hamasa kuhusu maswala mbalimbali ya maisha
utaweza kuhamasika zaidi.

Unapotumia muda wako kusoma vitabu,
ni wazi kuwa hutopata muda wa kupoteza, Kusoma vitabu kutakufanya utumie muda
wako kuongeza maarifa yako zaidi. Tofauti kubwa iliyopo kati ya kusoma vitabu
na kuangalia televisheni ni juu ya kuongeza ubunifu wako. Kusoma vitabu
hukufanya uondoke katika lindi kubwa la mawazo yanayokutesa na kukutafakarisha
juu ya mambo mengine. Waandishi wa vitabu hujenga mazingira ambayo msomaji
hujihisi yumo ndani yake.

Dakika mazungumzo yangu na Rc Mtaka
ananikumbusha kuwa “Mathias Kadri unavyosoma vitabu vingi kutoka kwa waandishi
mbalimbali, ndivyo unavyojitajirisha juu ya misamiati. Kuwa na ukwasi wa
misamiati husaidia sana katika maisha ya kila siku. Huongeza kujiamini na uwezo
wa kuzungumza mbele ya hadhira. Hadhira yoyote huvutiwa zaidi na mzungumzaji
mwenye kujiamini na mwenye uwezo wa kucheza na misamiati ya lugha kwa umaridadi
kadri ya muktadha.

Katika ziara hiyo niliondoka Mkoani
Simiyu nikiwa na kumbukumbu nzuri na umuhimu wa kukutana na Rc Antony Mtaka
nimeamini katika kusoma vitabu Unapata kujua mambo mapya, Ukuaji binafsi wa
weledi, kuongeza uelewa, na Kukupa msukumo wa kufanya Maandalizi kabla ya jambo
lolote.

Naamini sasa pamoja na mawazo chanya
ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe antony Mtaka unakubaliana na mimi kuwa kuna vito
vya thamani sana vilivyofichwa kwenye vitabu ambayo watu wengi hawavifahamu.

Ni muhimu ukajijengea utamaduni wa
kusoma vitabu mara kwa mara kadri uwezavyo. Unaweza kutumia programu kama vile
Balabolka ili kubadili vitabu kuwa sauti na uvisikilize badala ya kuvisoma.