Home Mchanganyiko WASTAAFU 10,000 WA PSSSF WALIOKUWA WANADAI MALIMBIKIZO YA PENSHENI YA MKUPUO NA...

WASTAAFU 10,000 WA PSSSF WALIOKUWA WANADAI MALIMBIKIZO YA PENSHENI YA MKUPUO NA ILE YA KILA MWEZI WAMELIPWA BILIONI 880

0

NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) umefanya malipo ya zaidi ya
shilingi bilioni 880 kwa wastaafu elfu 10,000 ambao walikuwa wanadai
malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ya kila mwezi, Meneja Kiongozi wa Mfuko
huo Bi. Eunice Chiume amesema.
Amesema
malipo hayo yamefanyika katika kipindi cha mpito kilichotolewa na serikali
kuanzia  Agosti 2018 hadi Februari 2019
hii ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu Mfuko huo uanze kutekeleza majukumu
yake Agosti 1, 2018 baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya
Jamii, ambayo ni PSPF,
LAPF, PPF na GEPF.
“Ili kuhakikisha PSSSF inatoa huduma bora na za haraka, imefungua
ofisi mikoa yote Tanzania bara na Visiwani na tunatoa wito sasa, kwa wale
wastaafu takriban elfu 10,500 ambao bado taarifa zao hazijahakikiwa wafike
kwenye ofisi zilizo karibu nao ili kukamilisha zoezi hilo muhimu linalofanyika
kila mwaka.” Alisema Meneja huyo kiongozi wakati akizungumza na waendesha
bloggers na waendesha mitandao ya kijamii kwenye ofisi za PSSSF, barabara ya
Ohio jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.
Alisema uhakiki wa wastaafu sio kitu kipya ingawa mwaka huu zoezi
hilo lilionekana kama ni geni.
“Lengo la uhakiki ni kuupa Mfuko fursa ya kufanya malipo kwa wakati, usahihi na kwa mtu anayepaswa kulipwa kwani taarifa zinaweza kubadilika ikiwa
ni pamoja na zile za kibenki huenda muhusika akahama kutoka benki moja kwenda
nyingine, mabadiliko ya wategemezi lakini haka kifo pia.” Alifafanua Bi.
Chiume.
 Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (katikati), akisikilzia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa bloggers katika kikao baina ya meneja huyo na wamiliki na waendeshaji wa blogu hapa nchini. Kikao hicho kilicholenga kujenga mahusiano na kuutambulisha Mfuko huo Mpya kwa wamiliki hao wa mitandao ya kijamii kilifanyika ofisi za PSSSF jengo la Jubilee Tower jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.
 Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akizungumza.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akizungumza.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi(kulia), akitoa maoni yake wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi. 
 Bi. Eunice Chiume (kushoto), akimsikilzia Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi (watatu kushoto), wakati wa kikao hicho.
 Bi. Eunice Chiume, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network, (TBN) Bw. Joachim Mushi, wakati wa kikao hicho.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (watatu kushoto) na Afisa Uhusiano Mewandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wakwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Bloggers mara baada ya kikao hicho.