Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa kwanza kushoto
na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma wa pili
kushoto, wakiwa kwenye kikao na Mkuu wa Wilaya (DC) ya
Nachingwea Rukia Muwango na kushoto kwake ni Afisa madini
mkazi mkoa wa Lindi Jeremiah Hango.
Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma akiwa chini
ya shimo kwa ajili ya kuchukua sampuli za mwamba wa madini ya
Graphate kwenye eneo la uchimbaji wa kampuni ya Lindi Jumbo
walipotembelea eneo linapo jengwa mgodi wa kampuni hiyo wilayani
Rwangwa.
Peter Malley Mjiolojia mwandamizi wa Kampuni ya Ngwena Tanzania
Ltd akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wake Prof. Kikula mara baada ya
kuwasili site kukagua maendeleo ya ujenzi wa mgodi wa kuchimba
madini ya Graphate.
*******************************
Na Issa Mtuwa (Wizara ya Madini) Nachingwea
Kamishna wa Madini Prof. Abdulkarim Mruma, amezitaka serikali za mitaa
hususani ofisi za wakuu wa wilaya kuwarasimisha maeneo wananchi
wanaogundua madini katika mfumo usio rasmi mara baada ya wananchi
hao wanapogundua madini kwa kuokota kwenye maeneo mbalimbali ili
kuepusha migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara baada ya wananchi
hususani wachimbaji wadogo na kisha kuvamiwa na wachimbaji na
wawekezaji wakubwa.
Prof. Mruma amesema hayo wakati wa mazungumzo baina ya Tume ya
Madini chini ya Mwenyekiti wake Prof. Idris Kikula na Mkuu wa Wilaya (DC)
ya Nachingwea Rukia Muwango walipo mtembelea ofisini kwake kwa
mazungumzo, na hiyo ni mara baada ya kumalizia kikao cha awali kilicho
ikutanisha baina ya viongozi wa juu wa tume ya madini na wafanyakazi wa
tume hiyo mkoa wa Lindi kwenye ofisi zao zilizopo wilayani Nachingwea
jana.
Prof. Mruma amesema serikali za mitaa zinawajibu wa kulinda haki ya
wananchi wanaogundua madini kwenye maeneo mbalimbali nchi ili kuwapa
umiliki kwa kuwatambua wenyewe binafsi na eneo ambalo madini hayo
huokotwa kabla ya kwenda kwenye ofisi za maafisa madini wa kazi waliopo
nchi nzima.
Amesema na kuongeza kuwa wananchi nao wanapogundua madini au
kuokota katika maeneo yasiyo rasmi hatua ya kwanza wakimbilie kwenye
ofisi za serikali za mitaa kwenda kuripoti na ofisi hizo mara moja
ziwatambue watu hao na mahali walipogundulia ili wasiporwe na wajanja.
“Naziomba serikali za mitaa hususani ofisi za wakuu wa wilaya
ziwarasmishe kwa kuwatambua wao wenyewe na eneo husika
walilogundua madini hayo ili kuleta udhibiti wa eneo kwa kuwatambua
wahusika mapema kabla ya mgogoro ya umiliki. Amesema mara nyingi
inapotokea hali kama hiyo kumekuwa na uwezekano wa wananchi
kuporwa haki ya umiliki wakati mwingine na vyombo vya serikali bila wao
kujiju hasa inapogundulika kuwa na madini wenye nguvu hukimbia mara
moja kukata leseni ya eneo hilo na kuanza kuwafukuza waliogundua au
wakati mwingine hata kuandikwa leseni jina la mtu asiyejulikana ili apewe
mwekezaji mkubwa.” amesema Prof. Mruma.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya amemshukuru prof. Mruma kwa kumpa
elimu hiyo ambayo amesema ni muhimu kwani kwa kufanya hivyo inalinda
haki ya mtu. Amesema hata Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
anathimini wagunduzi wa madini ndio maana alitoa Milioni 100 kwa
mgunduzi wa Tanzanite hivyo sisi pia tunao wajibu wa kuwalinda kwa
kuwarasmisha kwa kuwatambua wagunduzi hao ili maeneo hayo
yasivamiwe na wajanja.
Wakati huo huo Prof. Kikula na DC wamejadili changamoto ya uuzaji wa
madini yanayopatika mbali na soko la Nachingwea ambapo imebainika
kuwa wengi wao hupeleka Tunduru kuuzia madini yao. Katika kujadili
wameona kuwa endapo kama wachimbaji hao hakuna sababu ya kuwazuia
kwenda kuuza madini yao kwenye soko la Madini Tunduru linalotambuliwa
na serikali, haina shida chamsingi ni kuandaliwa utaratibu utakao
watambulisha wachimbaji hao na kupewa kibali ili mauzo yatakayofanyika
soko la Tunduru kwa madini yaliyotoka Nachingea rekodi zake zipelekkwe
Nachingwea na hilo linawezekana kwa kufanya mazungumzo baina ya
Ofisi ya Tume ya Madini Tunduru na ile ya Nachingwea ili kuwaondolea
usumbufu wachimbaji.