Home Uncategorized Rc Hapi apiga marufuku vifungashio vya mifuko ya Plastiki visivyo na nembo...

Rc Hapi apiga marufuku vifungashio vya mifuko ya Plastiki visivyo na nembo ya TBS

0

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamahuri Wiliam ( kulia) akimkabidhi jana mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi mifuko kilo 344 ya Plastiki ambayo imesalimishwa na wafanyabiashara wa Mufindi kwa ajili ya kuteketezwa ,mwenye sare za kijani ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Daud Yassin (picha na Francis Godwin)

Mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Mufindi katika viwanja vya mashujaa jana wakati wa kilele cha siku ya mazingira duniani ,maadhimisho yaliyofanyika kimkoa katika mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi (picha na Francis Godwin)

Mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi akionyesha jana wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani mjini Mafinga aina nyingine ya mifuko ya plastiki ambayo inatumiwa na wafanyabiashara ndogo ndogo mkoani Iringa kuwa vifungashio badala ya rambo ,mifuko ambayo pia ameipiga marufuku kuendelea kutumika (picha na Francis Godwin)

*****************************

NA Francis Godwin, Iringa
 Wafanyabiashara  mbali mbali wilayani Mufindi mkoani Iringa wamesalimisha   jumla ya  kilo 344 za  mifuko ya  Plasitiki  kwa ajili ya  kuteketezwa  ikiwa ni sehemu ya   kutekeleza  agizo la  serikali  la  upigaji  marufuku matumizi ya  mifuko  hiyo .
Akikabidhi  mifuko   hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi  jana wakati wa  madhimisho ya   siku ya mazingira  duniani  iliyofanyika   katika  viwanja  vya mashujaa mjini Mafinga  wilani Mufindi  kwa  mkoa wa Iringa,  mkuu wa wilaya ya  Mufindi  Jamhuri  Wiliam  alisema kuwa  mifuko  hiyo   imesalimishwa  katika   ofisi za Halmashauri  na  wafanyabiashara  hao kabla  kuanza kwa utekelezaji wa agizo la serikali na uzuiaji wa  matumizi ya mifuko  hiyo .
Mkuu  huyo wa  wilaya  alisema   kuwa  wilaya ya  Mufindi  iliweza  kutoa elimu kwa   wananchi  wake  juu ya  zuio la matumizi ya  mifuko  hiyo na   hadi  sasa   wananchi  wameanza matumizi ya  mifuko mbadala   inayotengenezwa  na  vikundi vya wajasiriamali kutoka ndani ya  wilaya  hiyo kwa  kutumia  karatasi kutoka  kiwanda cha Mgololo  kilichopo wilayani  hapo .
”  WAnanchi  wetu wa  Mufindi wameheshimu sana na kupokea  maelekezo ya serikali ya  kuanza matumizi ya  mifuko mbadala  lakini mkuu wa   suala   hili la mazingira  ni pana sana  na linagusa maisha ya wananchi  wetu  tunajua   suala la  kutunza vyanzo vya maji  tumekuwa  tukilipigia kelele   na  suala   hili bado lipo na tumekuwa tukiwapigia kelele   wananchi wetu kuhakikisha   wanaacha hatua tano kutoka  mito  pindi wanapofanya shughuli za  kilimo ”
Aidha  alisema  kuwa  wilaya  ya Mufindi wananchi  wanatumia sana mkaa na  kwa sasa  kupitia  viwanda   mbali mbali  vilivyopo  wilayani Mufindi   wameanza  utengenezaji wa mkaa mbadala  ambao  tayari unauzwa   kwenye maduka na maeneo mbali mbali ya  wilaya ya Mufindi na nje ya wilaya   hiyo  japo  bado kasi ya  uzalishaji wa mkaa huo ni  ndogo na haujaweza kuwatosheleza  wananchi wengi.
Hivyo  alisema   wananchi  wengi  wameendelea    kutumia mkaa wa  miti  ya  porini   na  kuwa  serikali  haijapiga marufuku matumizi ya mkaa wa porini  na  kuwa  wananchi wanaruhusiwa  kuendelea   kutumia mkaa  wa  porini na mkaa mbadala unaotengenezwa  viwandani  ila kinachotakiwa  ni kufuata  taratibu  za  ufanyaji wa biashara  ya  mkaa huo wa  porini pasipo  kuvunja  sheria.
Aidha  mkuu  huyo wa wilaya  aliwataka  wafanyabiashara  na  wananchi  wa  wilaya ya  Mufindi   kuendelea  kutekeleza  agizo la   serikali la   utumiaji wa mifuko mbadala  na  kuepuka  matumizi ya mifuko ya  plastiki ambayo  tayari imepigwa marufuku huku  akiwataka  wale ambao  bado hawajasalimisha  mifuko  ya plastiki katika ofisi za Halmashauri  ama  ofisi za  watendaji wa  mitaa na kata  kufanya hivyo kwani  kukutwa na mifuko hiyo ni  kosa  kisheria na  mtumiaji anaweza  kufungwa  jela siku saba ama  faini .
Kwa  upande wake  mkuu wa  mkoa wa Iringa Alli Hapi  mbali ya  kupongeza hatua  iliyochukuliwa na wafanyabiashara na  watumiaji wa  mifuko ya  plastiki wilayani Mufindi  kwa  kukabidhi kilo   344 za mifuko  hiyo  kwa   ajili ya  kuteketezwa  bado  aliziagiza  halmashauri  zote za  mkoa wa Iringa  kuendelea  kutoa   elimu na  kuwachukulia  hatua   wale  wote  ambao  wanatumia  mifuko ya plastiki mweupe  kwa   kufungashia  bidhaa ambazo  hazijawekewa nembo ya  ubora  na TBS .
Kuwa   baada ya  serikali  kuzuia matumizi ya  mikofo ya rambo na mingine ya plastiki yenye rangi  baadhi ya  wananchi wameanza  kutumia mifuko  ya plastiki  mweupe  kwa  kugeuza kama  kifungashio  kuwa  kufanya  hivyo ni  kosa na mifuko  hiyo  nayo haitakiwi ila  vifungashio  vinavyoruhusiwa ni  vile ambavyo  vimewekewa  alama ya  ubora  na TBS pekee .
Alisema  kutokana na na wajasiriamali  wanawake  katika  wilaya ya Mufindi wameanzisha   vikundi vya utengenezaji wa mifuko mbadala  kwa matumizi ya  kubebea  bidhaa mbali mbali  ni  vizuri  halmashauri  za wilaya ya  Mufindi   kuwasaidia  mikopo isiyo na riba   ili  kuongeza mitaji na  kutafuta mashine  za  kutengenezea  mifuko   hiyo  na  ikiwezekana   waweze kuisambaza  wilaya  nzima  mkoa na nje ya  mkoa wa Iringa .