MWENYEKITI wa Bodi ya wadhamini ya Chama Cha walimu Tanzania (CWT), Bw.Clement Mswanyama,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa za chama hicho.
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MWENYEKITI wa Bodi ya wadhamini ya Chama Cha walimu Tanzania (CWT), Clement Mswanyama,amewataka walioshindwa katika chaguzi za uongozi wa nafasi mbalimbali katika Chama hicho kuacha kutoa habari za kupotosha watu.
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kichwa cha habari kilichochapishwa katika gazeti fulani la hapa nchini kilichokuwa kinasomeka “CWT KWAWAKA”.
Bw.Mswanyama amesema kuwa katika gazeti hilo waandishi wake walieleza majengo na mali za CWT ,kampuni tanzu ya CWT na TDCL na Benki ya Mwalimu (MCB) kuwa si mali ya walimu jambo ambalo Ni uongo wenye nia ya kuchochea .
Aidha amesema kuwa katiba ya CWT toleo la sita la mwaka 2014 inasema kuwa Mali za chama zitaandikishwa kwa jina la Bodi ya wadhamini pia mikataba yote,hati na dhamana za fedha za chama zote zitamilikiwa kwa jina la Bodi ya wadhamini na kuhifadhiwa kwa katibu mkuu wa CWT.
“Tulizipata taarifa hizo za gazeti kwa masikitiko makubwa na tukajiuliza wenzetu hao wamepata maelezo kutoka kwanani na kwadhamira ipi” amesisitiza Bw.Mswanyama
Hata hivyo amesisitiza kuwa suala hili tunahitaji kuhojiana nao kwa kina na ikibainika wamepotosha umma na walimu kwa ujumla ni lazima tutachukua hatua za kisheria.
Bw.Mswanyama amelitaka gazeti hilo kuomba radhi kupitia gazeti lao na Kama wakishindwana watachukua hatua za kisheria juu yao.
” Ni kweli gazeti hilo lilinukuu ripoti maalum ya mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) aliyekagua CWT katika mwaka wa fedha 2016/2017
Amesema kuwa mpaka leo tunawahakikishia walimu tumeyafanyia kazi kwa asilimia kubwa na tunaendelea na zoezi hilo kwani ushauri mwingine ulihusu taratibu za kila siku za uendeshaji wa Chama na matumizi ya Mali za fedha za chama.
Kwa upande mwingine Bw.Mswanyama ametolea ufafanuzi kuhusu Teachers Development Co.Ltd (TDCL) amesema kuwa kampuni ambayo ilianzishwa na CWT mahususi kwa ajili ya kusimamia uwekezaji unaofanywa ndani ya Chama.
Amefafanua kuwa CAG alipofanya ukaguzi Maalum ndani ya CWT alibaini kuwa kampuni ya TDCL ni Mali ya CWT isipokuwa hayakuwepo makabidhiano rasmi ya usimamizi wa kampuni hiyo.
Aidha amezungumzia kuhusu Benki ya Mwalimu na kusema kuwa inamilikiwa na walimu kwa asilimia 51.35 na kutoa mchanganuo wa Umiliki wa hisa.
Bw.Mswanyama amesema kuwa mchanganua huwa kuwa ni CWT Umiliki hisa 12.94, TDCL hisa 3.23 na Walimu hisa 35.18 ambapo jumla asilimia 51.35 na zingine ni PSPF (PSSSF) 16.17,NHIF 16.17 na Public 16.31 jumla 48.65.
Na pia amezungumzia Mwalimu house na kusema kuwa ni kitega uchumi cha Chama ambacho kilijengwa kwa kutumia mapato ya asilimia mbili za wanachama .