*********************************

Na Ahmed Mahmoud Arusha

JESHI la polisi mkoa wa Arusha linawashikilia watu kadhaa akiwemo Mwalimu wa shule ya Msingi kwa kukutwa na Bunduki AK 47 anayoitumia katika matukio ya uhalifu ikiwemo ujangili na biashara ya silaha, 

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana,  amemtaja Mwalimu huyo kuwa  ni Solomoni Letato Kipuker miaka (30 )  ambae ni mwalimu  wa shule ya msingi Naan, iliyopo kata ya  Engusero sambu tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro amekamatwa Juni 2 mwaka huu akiwa na bunduki pamoja na magazine yenye risasi tano.

Amesema Kuwa mwalimu huyo amekamatwa  kwa ushirikiano wa  wa kikosi kazi  kambambe  na Jasiri dhidi ya ujangili  na uhalifu wa silaha za moto  kanda ya Ziwa  chini ya uwezeshaji wa Tanapa  kwa tuhuma za kuhusika na ujambazi,kukamatwa na nyara za serikali.

Amesema mtuhumiwa huyo ni miongoni mwa wafanyabiashara  haramu ya  uingizaji silaha za moto  nchini pamoja na biashara ya nyara za serikali  hasa meno ya Tembo  na Pembe za Faru  na shughuli zingine za ujangili na Ujambazi na utekaji watalii  na wananchi

Kamanda Shana,amesema jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha moja  ya AK 47 iliyotelekezwa kwenye ofisi ya kijiji cha Mbukeni kata ya Arash tarafa ya Loliondo, baada ya kuwepo kwa taarifa za Kiintelejenisia ikiwa na risasi moja na watuhumiwa wanatafutwa.

Amesema mara baada ya kumhoji mtuhumiwa huyo alikiri kujihusisha na vitendo hivyo  kwa kushirikiana na watuhumiwa wengine ambao wametoroka  na wanatafuta na pia silaha hiyo imekuwa ikitumika kwenye mapigano  ya kikabila kati ya Maasai, Wasonjo na Watemi, wilayani Ngorongoro.

Amesema jeshi la polisi linampongeza Kamishina  wa Uhifadhi Tanapa, Dakta Allan Kijazi  kwa ushirikiano mkubwa ambao jeshi lake la kupambana na ujangili limekuwa likitoa.

katika tukio lingine jeshi la polisi  limefanikiwa kuwakamata majangili  sugu  na hatari wakiwa na nyara za serikali  May 30 mwaka huu katika kitongoji cha Maji ya Chai tarafa ya King’ori wilayani Arumeru .

Amesema majangili hao watatu ambao majina yao yamehifadhiwa  baada ya kuhojiwa wamekiri kuhusika  kujihusisha na  biashara  hiyo ya ujangili.

 Amesema majangili hao wamekamatwa wakiwa na vipande  vine vya meno ya Tembo  walivyokuwa wamefihifadhi kwenye mfuko wa  Sandarusi .

Katika tukio lingine jeshi la polisi limefanikiwa kukamata  watuhumiwa watatu  wa wizi wa pikipiki  ambao amewataja kuwa ni Hamis Juma (37) mkazi wa Olmatejoo jijini Arusha, Isiaka Islam (22) mkazi wa Majengo mkoani Kilimanjarona Hassan Mushi (54) mkazi wa  Majengo mkoani Kilimanjaro.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi linamfikisha mahakamani jambazi Jumanne Mjusi ambae alikamatwa wiki iliyopita akwa na bastola baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda, Shana ,amewaonya wananchi mkoani Arusha wanaojihusisha na uhalifu wa aina yeyote kuacha mara moja vinginevyo watatiwa mbaloni bila kujali rangi, jinsia,dini wadhifa alionao mhusika.