Home Mchanganyiko TPDC WATAKIWA KUHAKIKISHA MAGARI WANAYOAGIZA YAWE YANATUMIA MFUMO WA GESI

TPDC WATAKIWA KUHAKIKISHA MAGARI WANAYOAGIZA YAWE YANATUMIA MFUMO WA GESI

0

Mmoja wa wafanyakazi wa TPDC akimuelezea Waziri Angela Kairuki namna wanavyojitahidi kufanya kazi katika shirika hilo katika maadhimisho ya miaka 50 ya shirika la TPDC.

TheVoicetz wanaojihusisha na kuimba katika majukwaa wakiwa wanatumbuiza katika maadhimisho ya miaka 50 ya shirika la TPDC yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

*******************************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Uwekezaji Mh.Angela Kairuki amewataka wafanyakazi wa shirika la maendeleo ya mafuta na petroli nchini(TPDC) pamoja na Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa  magari wanayoagiza kwa ajili ya matumizi ya shughuli za serikali yawe yamefungwa mfumo wa kutumia gesi ili kuwa mfano wa kuigwa na wengine ili kukuza sekta ya gesi asilia.

Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya shirika hilo toka kuanzishwa kwake mwaka 1969 na baba wa Taifa Mwalimu  Julius Nyerere kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo.

“TPDC mnauwezo wa kulifikisha taifa katika uchumi wa kati hivyo nasi tutaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha tunafanikiwa kwa hilo”. Amesema Mh. Angela.

Pia ameiagiza TPDC kuzipitia upya bei za gesi kwenye viwanda ili kuchochea uwekezaji sekta ya viwanda kwani kwa sasa asilimia 60 ya umeme katika gridi ya Taifa inatokana na umeme wa gesi asilia.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati  Mh. Medadi Kalemani amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika gesi ili kuweza kukuza uchumi wa nchi ambapo viwanda navyo vinategemea nishati kuendesha viwanda vyao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kwa mwaka huu wa Fedha unaoishia juni  Shirika hilo linatarajia kupata faida ya shilingi billion 9 na kuacha kujiendesha kwa hasara na hatimaye kutoa gawio kwa Serikali.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa  tayari magari 200 yanatumia mfumo wa nishati ya gesi pamoja na Viwanda 44 ambavyo vinatumia nishati hiyo,huku jitihada mbalimbali bado zinaendelea kuhakikisha kuwa gesi inafika kwenye maeneo mengi hapa nchini

Hata hivyo ameongeza kuwa  kunauhitaji mkubwa wa usambazwaji wa gesi ila kwa sasa wanaenda taratibu kutokana na upatikanaji mdogo wa fedha huku asilimia 60 ya Umeme unaotumika kwenye gredi ya taifa unatokana na gesi asilia.