Maafisa Viwango wakiongozwa na Meneja wa Viwango TBS, Bw.Yona Afrika wakimsikiliza mbuni wa gari la kutumia umeme Masoud Kipanya mara baada ya kutembelea karakana ya mbunifu huyo iliyopo SIDO Jijini Dar es Salaam kuona ubunifu uliofanywa na mbunifu huyo. Meneja wa Viwango TBS, Bw.Yona Afrika akizungumza mara baada ya kutembelea karakana ya mbunifu Masoud Kipanya iliyopo SIDO Jijini Dar es Salaam kuona ubunifu uliofanywa na mbunifu huyo.Kaimu Meneja wa Udhibiti Ubora, Baraka Mbajije akizungumza mara baada ya kutembelea karakana ya mbunifu Masoud Kipanya iliyopo SIDO Jijini Dar es Salaam kuona ubunifu uliofanywa na mbunifu huyo. Mbunifu wa gari la umeme Masoud Kipanya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelewa na Shirika la Viwango Tanzania katika karakana yake iliyopo SIDO Jijini Dar es Salaam.
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limemtaka Mtanzania mbunifu Masoud Kipanya kufika katika ofisi za TBS na gari la kutumia umeme alilolibuni hivi karibuni ili liweze kukaguliwa na baadae aweze kupata leseni na cheti cha ubora wa viwango.
Wito huo umetolewa leo Aprili 14,2022 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Viwango TBS, Bw.Yona Afrika wakati walipotembelea karakana ya mbunifu Masoud Kipanya SIDO ili kuona ubunifu alioufanya kwa kutengeneza gari la kutumia umeme.
Bw.Yona amesema wameangalia kwenye maktaba ya kitaifa wakajihakikishia viwango vya upimaji wa magari ya umeme vipo na ndivyo ambavyo watavitumia kukagua gari hilo la kisasa ili kuona hatua ya mwisho ya kupewa leseni na TBS ya Ubora wa gari linalotumia umeme Tanzania inatoka.
“Lengo hasa ni kutaka kuangalia hili gari linakidhi viwango, kwahiyo hatua ya kwanza ambayo tutaifanya kwasababu mpaka tunakuja hapa tuliwasiliana na Masoud Kipanya pindi tu alipotangaza na kutusisitizia ngoja kwanza amalizia matengenezo ili itakapofika kipindi atakapotaka leseni ndo tweze kujiridhishe”. Amesema Bw.Yona.
Kwa upande wake mbunifu wa gari hilo Masoud Kipanya ameipongeza TBS kwa kazi wanayoifanya hivyo atajitahidi kuafanyia kazi yale yote ambayo ataelekezo na TBS ili kuweza kutimiza malengo yake.
Aidha Masoud Kipanya amewashauri wabuni wengine waliopo mitaani waweze kujitokeza na kufika TBS ili waweze kukaguliwa bidhaa zao ambazo wamebuni na kuweza kutimiza malengo yao.