Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Dkt ,Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa ABBOT Fund Tanzania Bi.Natalia Lebou,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu WIzara ya Afya- Idara Kuu ya Mmaendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi na Wanafunzi waliohidhuria wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango,(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akiangalia Ramani na kupata maelezo kutoka kwa Msanifu wa Majengo David Kibebe kuhusu ujenzi wa Nyumba za Makazi na Huduma mbalimbali, Wakati wa Uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma. wa pili kulia Dkt. Doroth Gwajima (MB) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto. kushoto ni Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizindua Makao ya Taifa ya Watoto iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Mpango,akipanda Mti wa Matunda baada ya kuzindua Makao ya Taifa ya Watoto iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Muonekano wa Kituo cha Makao ya Taifa ya Watoto kilichozinduliwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akisalimiana na Watoto wanaotunzwa katika Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akiagana na Watoto wanaotunzwa katika Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto leo Juni 16,2021 yaliyofanyika katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akiagana na Bibi Natalia Lebou Mkurugenzi wa Abbot Fund Tanzania Watoto wanaotunzwa katika Makao ya Taifa ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika na Uzinduzi wa Makao ya Taifa ya Watoto leo Juni 16,2021 yaliyofanyika katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Makao ya Taifa ya Watoto iliyoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, iliyoadhimishwa leo Juni 16,2021 katika Kijiji cha Kikombo Jijini Dodoma.
Picha Na.Alex Sonna pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais
………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MAKAMU wa Rais wa Tanzania,Dkt Philip Mpango ameishauri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,kupitia upya masharti ya utaratibu wa kuasili watoto ili kuhamasisha watanzania na watu wengine wenye nia njema kuasili watoto hivyo kupunguza idadi ya watoto kwenye makao.
Akizungumza leo June 16,2021 wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya watoto katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma,Makamu wa Rais ameiomba Wizara hiyo kupitia upya utaratibu huo ili kuwapa nafasi watanzania kuasili watoto ambao wanaishi kwenye makao hayo.
“Naomba kutumia fura hii kuishauri Wizara kupitia upya masharti ya utaratibu wa kuasili watoto ili kuhamasisha watanzania na watu wengine wenye nia njema kuasili watoto hivyo kupunguza idadi ya watoto kwenye makao,”amesema Dk.Mpango.
Hata hivyo,Dkt.Mpango amewasihi watanzania wenye uwezo kuguswa na maisha ya watoto wanaishi kwenye mazingira hatarishi na wachukue hatua kuasili watoto na kuwatunza kwa upendo kwa mujibu wa mila na tamaduni hususani pale inapotokea watoto wa ndugu kufiwa na wazazi.
Vilevile,amewashukuru viongozi wa dini kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kufundisha na kusimamia maadili mema katika jamii huku akisisitiza viongozi hao kuendelea kulifanya suala hilo kama agenda ya kudumu katika nyumba za ibada na katika mikusanyiko ya kidini.
“Nawapongeza wasimamizi wote wa vituo vya kutunza watoto kwa moyo wao wa kujitolea wa kuwalea watoto wetu.Serikali inatambua mchango wenu katika malezi ya watoto wetu na naomba kuwatia moyo muendelee na jukumu hili na Mwenyezimungu atawabariki,”amesema.
Awali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Dkt ,Dorothy Gwajima amesema Juni 16 ni siku ya mtoto wa Afrika ambapo nchi zote wanachama wa Umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania wanaadhimisha siku hiyo.
Amebainisha kwamba kama sehemu ya maadhimisho hayo serikali imezindua Makao ya watoto ya Kikombo Mkoani Dodoma ambapo ameitaka jamii kufanya tathmini ni sababu ipi inayopelekea watoto wa mitaani kuongezeka.
Hata hivyo amesema Ujenzi wa Makao hayo unatarajia kuwezesha serikali kutatua changamoto za huduma katika Makao ya watoto kwani kituo cha Kurasini ni kidogo.
Hata hivyo ameeleza kuwa , Ujenzi wa Makao ya Taifa hayo ya watoto yamegharimu Jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni 5.5 Sawa Shilingi bilioni 12.7 za kitanzania ambapo mpaka sasa makao Makuu hayo yanawatoto 28 ambao wanaume ni 16 na watoto wa kiume ni 12.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo amesena kuwa kuna tatizo kubwa sana la watoto wa mitaani waliokosa malezi bora hivyo anaamini kupitia kuwepo kwa kituo hicho kutaleta matokeo chanya.
“Tuna watoto mil.20 lakini mil. 3 wanaudumavu hivyo tunahaja yakutoa elimu kwa familia”amesema Nyongo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Antony Mavunde amesema inapofika majira ya jioni katika eneo la Nyerere Square watoto wengi hutandika mabox na kulala chini.
“Ujenzi wa kituo hiki naamini watanufaika maana wengine wanatumia gundi na madawa ya kulevya”amesema Mhe.Mavunde