Home Mchanganyiko RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. HUSSEIN ALI MWINYI AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA SEKTA...

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. HUSSEIN ALI MWINYI AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA SEKTA WA WATEMBEZA WATALII ZANZIBAR.

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watembeza Watalii Zanzibar (ZATO) Bw. Hassan Ali Mzee, akjitowa maelezo ya Jumuiya yao wakati wa mkutano wao na Rais ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake na Sekta mbalimbali za Wafanyabiashara Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

KATIBU Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bi. Fatma Mbarouk Khamis akizungumza na kutowa ufafanuzi wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wafanyabishara wa Sekta ya Utalii Zanzibar, ikiwa ni muendelezo ya mikutano yake, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kulia kwake) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe Lela Mohammed Mussa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)

Mkurugenzi Masoko Kamisheni ya utalii Zanzibar, Dkt Miraj Ukuti Ussi akizungumza wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokutana na Wafanyabiashara Sekta ya Watembeza Watalii Zanzibar (ZATO) ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake na Wafanyabiashara Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi  Mhandisi Zena Ahmed Said akizungumza wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wafanyabiashara ya Sekta ya Watembeza Watalii Zanzibar (ZATO)  uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu  na (kushoto kwake) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa .(Picha na Ikulu)

MFANYABIASHARA wa Sekta ya Watembeza Watalii Zanzibar Bw. Mohammed Salim akichangia wakati wa mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake na Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali Zanzibar.(Picha na Ikulu)