Home Mchanganyiko KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA IMERIDHISHWA NA...

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA IMERIDHISHWA NA UKARABATI WA SHULE KONGWE YA WAVULANA YA KIBAHA

0
……………………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KAMATI ya Bunge ya Kudumu Utawala na Serikali za Mitaa imeridhishwa na ukarabati wa shule kongwe ya wavulana ya Kibaha,pamoja na mfumo wa malipo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Humphrey Polepole akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea Shirika la Elimu Kibaha (KEC) kuangalia miradi inayotekelezwa na serikali ambayo ni ya shule na hospitali ambazo ziko chini ya shirika hilo.
Polepole alisema ,shule hiyo ilipewa zaidi ya sh.bilioni moja ambazo zimetumika vizuri na kuonyesha mwonekano mzuri wa shule hiyo kongwe.
“Tumeridhishwa na ukarabati uliofanyika kwa shule hii ambayo baadhi ya viongozi mbalimbali wa serikali wamesomea hapa na hii itaifanya elimu kuboreka,” alisema Polepole.
Aidha alisema kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi mfumo wanaoutumia wa malipo ya serikali umeboresha kuongeza mapato na kuboresha mapato.
“Hata hivyo naomba serikali iendelee na maboresho ya mfumo wa malipo hayo ili kuondokana malipo ya fedha taslimu na badala yake uwe wa kieletroniki moja kwa moja bila ya changamoto zilizopo sasa,” alisema Polepole.
Naye Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde alisema kuwa serikali imeweka mpango mkubwa wa wananchi wote kuwa na bima ya afya na kuepukana na malipo ya fedha taslimu.
Awali mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 4.7 kwa shule tano kongwe ikiwemo Kibaha pia Ruvu sekondari milioni zaidi ya 900, Minaki milioni 500, Bagamoyo zaidi ya milioni 900, Kibiti bilioni 1 ambapo pamoja na fedha za elimu bure mkoa umepata bilioni 42.9.
Akizungumzia mfumo wa malipo kwenye hospitali ya Tumbi ,Ndikilo alieleza, mapato yalikuwa 300,000 hadi sasa milioni tatu kwa siku.
Hospitali hiyo ina vitanda 250 na inapokea wagonjwa kutoka mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Morogoro.