Mkuu wa Taasisi wa Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa tiba katika hospitali ya Palestina-Sinza katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya Ustawi Ustawi wa Jamii wakiwa katika Hospitali ya Palestina wakati walipopeleka msaada wa vifaa tiba katika hospitali hiyo.
Sehemu ya Vifaa Tiba vilivyotolewa katika Hospitali ya Palestina na Wafanyakazi Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
***************************
Wafanyakazi Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii imetoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali katika hospitali ya Palestina-Sinza ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutambua kama wanawake wanawajibu wa kuunga mkono serikali katika sekta ya afya.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa tiba hivyo Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni amesema kuwa vifaa tiba hivyo vimetokana na mchango wa wananwake wa Taasisi hiyo kwa kuamini wanaweza bila kuwezeshwa.
Amesema kuwa vifaa tiba walivyotoa wanaamini kuwa vitasaidia katika mahitaji ya Hospitali kwa kuhudumia wagonjwa wanaofika hapo.
“Sisi wanawake tunaweza ndio maana baada ya kutambua siku ya wanawake duniani inakuja tukajichanga kutoka mifukoni mwetu ili kuweza kufikia azima ya kununua vifaa tiba na kufikisha katika hospitali ili ndugu,jamaa na watoto wanaofika kuweza kutumia”amesema Dkt.Nyoni.
Nae Mratibu wa Huduma Tiba wa Hospitali ya Palestina-Sinza Dkt.Nchang’wa Nhumba amewapongeza wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kutambua Palestina wanahitaji msaada kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika katika hospitali hiyo.
Dkt.Nhumba amesema kuwa Wanawake wa Ustawi wa Jamii waendelee kuwa na moyo huo hata wakati mwingine waweze kwenda kusaidia na kuongeza kuwa wanawake wa Taasisi zingine kuiga mfano huo.