Alfred Mwakalebela akizungumzia na wanahabari.
picha za ajali iliyotokea alfajiri ya leo eneo la Mseke Uyole  Iringa vijijini barabara kuu ya Iringa -Mbeya
……………
NA DENIS MLOWE, IRINGA
WATU wawili ambao wote madereva asubuhi ya leo wamepoteza maisha kufuatia ajali mbaya iliyotokea katika eneo la Mseke barabara kuu ya Iringa -‘ Mbeya baada ya kugongana uso kwa uso na basi kutumbukia mtoni.
Katika ajali hiyo iliyohusisha basi la kampuni ya Classic linalofanya safari zake kati ya Harare nchini Zimbabwe na Dar es Salaam Tanzania.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa,
Daktari Alfred Mwakalebela, wapokelewa majeruhi 13 hospitalini hapo ambapo wanawake watatu na wanaume kumi.
Daktari Mwakalebela amesema kuwa watu watatu wako katika hali mahututi, akiwemo mwanamke mmoja mjamzito aliyepata kuvunjika mgongo.
Mwingine amejeruhiwa mbavu na kupata kutokwa damu ndani ya kifua, huku mwingine akiwa na mivunjiko ya kawaida.
Mwakalebela alisema kuwa majeruhi Wote 13 wamelazwa kwa uangalizi maalum wa madaktari.
Katika wale waliofariki mtu mmoja ambaye ni Mtanzania anayeripotiwa kuishi katika eneo la Tunduma amefahamika na majeruhi raia wanne wa Zambia, na raia wanane wa Zimbabwe.
Daktari Mwakalebela amesema hali za majeruhi zinaendelea kufuatiliwa, na baadhi yao huenda wakaruhusiwa kuanzia kesho kutwa endapo hali zao zitaimarika.
Katika hali taarifa nyingine Mwakalebela akizungumzia majeruhi wa ajali iliyopita ya basi la Shabiby na roli iliyotokea Wiki iliyopita amesema majeruhi wawili kutoka ajali iliyopita bado walikuwa wakihudumiwa mmoja akiwa na jeraha la jicho lililokuwa likimaliziwa kushonwa leo, na mwingine akiwa tayari kufanyiwa upasuaji kutokana na mivunjiko.