Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi (katikati) akiwa ameshikilia mfano wa mtungi wa gesi kuashiria uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pamoja naye kulia ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Bw. Mohammed Albeiiti, kupitia ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza jukwaani kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Bw. Mohammed Albeiiti pamoja na Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni, kupitia ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.
Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza jukwaani wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Bw. Mohammed Albeiiti, kupitia ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Mohammed Albeiiti akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza jukwaani wa kwanza katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi pamoja na kushoto ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni, kupitia ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi (katikati) akiwa ameshikilia mfano wa mtungi wa gesi kuashiria uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini ambapo kwa siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.
Wateja wa Vodacom Tanzania na Gas Fasta wamerahisishiwa upatikanaji wa gesi kupitia ushirikiano wa kampuni hizo mbili unao wawezesha kuagiza, kulipia na kisha kufikishiwa mitungi ya gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.
Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi ushirikiano huo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi amepongeza jitihada zinaonyeshwa na sekta binafsi kwa kutumia ubunifu wao wa kidigitali katika kuunga mkono juhudi za serikali ambao utaongeza hamasa ya Watanzania kutumia gesi asilia na rafiki kwa utunzaji wa mazingira nchini kote.
“Niwapongeze M-Pesa na Gas Fasta kwa ushirikiano huu muhimu ambapo mmeamua kuunganisha nguvu kuwarahisishia Wateja wenu kupata huduma ya gesi kwa njia ya kidigitali. Tukio hili halitokuwa na manufaa kwa wateja wenu pekee pia na kwa Watanzania wote kwa ujumla kwa sababu wote wanapendelea upatikanaji wa huduma na bidhaa kwa usalama, uharaka, na unafuu kuendana na maisha yao ya kila siku. Kama serikali, tunafanya jitihada kubwa kwa kushirikiana na wadau tofauti nchini kuongeza nguvu ya kujenga hamasa na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya gesi asilia ambayo ni rafiki kwa utunzaji wa mazingira. Nitoe wito kwa ushirikiano wa namna hii katika maendeo mbalimbali ili kufikia malengo yetu ya Watanzania wote kutumia gesi asilia kwa manufaa ya afya na uchumi wa taifa lote kwa ujumla,” alisema Mh. Katambi.
Akielezea umuhimu wa ushirikiano na Gas Fasta uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni amesema kuwa huu ni mwendelezo wa jitihada zao za kuifanya aplikesheni ya M-Pesa kujitosheleza na kuwawezesha Watanzania kuitumia kwa manunuzi na malipo ya huduma na bidhaa mbalimbali kwa kidigitali.
“Tunayo furaha kuwakaribisha Gas Fasta katika familia ya M-Pesa Super App. Kama tulivyowafahamisha wakati tukiizindua, lengo letu ni kuifanya M-Pesa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya watanzania yaani ‘Digital Lifestyle App’ huku ikichochea mapinduzi ya uchumi wa kidijitali nchini. Hii ina maana kuwa siku zijazo wateja hawatokuwa na haja ya kuwa na utitiri wa aplikesheni za huduma tofauti katika simu zao, kwani M-Pesa pekee itajitosheleza kukidhi mahitaji yao. Ushirikiano wetu na Gas Fasta ni wa kipekee sana kwani unaenda sambamba na malengo yetu mapana kama Vodacom Tanzania kwenye utunzaji wa mazingira. Vile vile kama hii haitoshi, katika siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa hadi shilingi elfu kumi papo hapo pindi atakapofanya manunuzi ya gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa” alisema Bw. Mbeteni.
Aidha Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba muundo wa M-Pesa wa uundaji wa thamani (yaani value creation model) umejikita katika kushirikiana na jamii zilizowazunguka pamoja na wadau mbali mbali katika kufanikisha utoaji wa huduma zao. Falsafa hii imewawezesha kutengeneza ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa watanzania takribani 1,000 pamoja na kushirikiana na taasisi za serikali na sekta binafsi katika malipo na makusanyo hivyo kuchochea ukuaji wa kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Mohammed Albeiiti, amebainisha kuwa, “ni furaha na heshima ya kipekee kushirikiana na M-Pesa, huduma iliyoleta mapinduzi ya ujumuishaji wa huduma za kifedha nchini na ukanda wote wa Afrika ya Mashariki. Huduma yetu ya Gas Fasta ilianzishwa baada ya kutambua usumbufu na upotevu wa muda na gharama wanaoupata Watanzania pindi wanapoishiwa na gesi, na mara nyingi wakati wakipika. Kama tunavyofahamu, huwezi kumwaga chakula au ukaenda kununua kingine pindi ukiishiwa na gesi, suluhisho ni kuagiza mtungi mwingine. Na hapo ndipo sisi tulipokuja na suluhisho la kidigitali, kwa kutambua idadi kubwa ya watu wanatumia simu janja, tukaona ni fursa ya kuwafikia muda na mahali popote walipo kwa uhakika na usalama zaidi. Tuna matarajio makubwa kupitia ushirikiano huu na ukubwa wa M-Pesa kutokana na teknolojia, uzoefu na rasilimali zake hususani yanapokuja masuala ya kidigitali maana yenyewe ni huduma ya kidigitali na siku zote inafikiria kidigitali zaidi.”
Kupitia Gas Fasta, mtumiaji anaweza kufanya manunuzi ya gesi na kufikishiwa alipo kutoka kwa wasambazaji wote wa gesi za kupikia nchini na hivyo kuchangia utunzaji wa mazingira kupitia matumizi ya nishati safi ya kupikia. Hali kadhalika, kupitia aplikesheni ya M-Pesa, watumiaji wamewezeshwa kufanya manunuzi na malipo kwenda kwa watoa huduma takribani 20 ikiwemo tiketi za usafiri wa anga, vifurushi vya televisheni, malipo ya bidhaa kidogo kidogo na nyinginezo nyingi.