Na: Neema Adriano
TARI Ilonga imekuja na Teknolojia mbalimbali ambazo zinazalishwa na kituo Cha Ilonga pamoja na vituo mbalimbali hasa vituo vilivyopo Kanda ya Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti,6, 2023,katika Viwanja vya Nanenane Morogoro Mratibu wa Kitaifa wa utafiti wa Mtama,Ulezi na Uwele, Bw.Emmanuel Thomas Mwenda amesema wamewaletea wakulima Teknolojia ambayo utawasaidia kupata mavuno yenye tija.
Amesema mazao mengi ambayo wameyaleta katika Viwanja hivyo yamelimwa na wakulima katika maeneo ya Kanda ya Mashariki ikiwemo mazao ya Mtama, Ulezi na Uwele pamoja na mazao mengine mengi.
“Teknolojia kubwa ambazo tumezileta Moja ni mbegu Bora lakini pili ni kanuni bora za kiagronomia ambazo tunamshauri mkulima aweze kuzitumia ili aweze kuzalisha kwa tija.
“Mbegu tulizozoleta kwa zao la Ulezi timeleta mbegu tatu zilizo Bora na zilizotafitiwa na zina tija kubwa,mbegu hizi ni P224,U15 pamoja na TARI FM1,mbegu hizi tatu zina uwezo wa kuzaa kuanzia Tani 2 mpaka Tani 4 kwa heka moja haya ni mavuno makubwa sana ukilinganisha na mbegu zile za kienyeji ambazo tunazitumia.
Ameendelea kusema kuwa kwa upande wa zao la Mtama wameleta mbagu ya masia ambayo ni Mtama mweupe,mbegu ya TARI SOR2 ambayo pia mi Mtama mweupe na mbegu ya TARI SOR 1 ambao wenyewe una rangi ya kahawia.
“Hizi ni mbegu Bora ambazo zina sifa tofauti tofauti nikianza na mbegu aina ya masia yenyewe Ina uwezo wa kutoa Rani 3.5 mpaka Tani 4 kwa heka Moja yaani magunia 35 mpaka 40 kwenye heka Moja endapo mkulima atatumia kanuni bora za kiagronomia,mbegu hii Ina uwezo wa kuzaa vizuri kuanzia ukanda wa chini mpaka ukanda wa kati na Ina uwezo wa kutoa mavuno hayo niliyoyasema.
Pia Bw. Mwenda amesema Mbagu ya TARI SOR2 yenyewe Ina uwezo wa kuzaa tani 3 mpaka Tani 3.6 kwa heka Moja na mbegu hiyo Ina sifa ya ziada ya kuweza kukabiliana na gugu chawi aina ya kiduha ambayo inasumbua sana katika maeneo ambayo yana upungufu sana wa rutuba au eneo lenye kichanga.
“Njia shirikishi ambayo unaweza kuitumia katika kukabiliana na gugu chawi hili mojawapo ni kutumia mbegu zenye ukinzani na gugu hilo ambao ni kama hii niliyoisema.
Ameeleza kuwa njia nyingine ya pili ni pamoja na matumizi ya mbolea hasa samadi lakini pia namna Bora ya kufanya kilimo Cha mzunguko lakini njia hii Sasa ya kutumia mbegu ambayo yana ukinzani inaonekana kufanya vizuri zaidi kwa wakulima ambao Wana ardhi ndogo ambayo wanaitumia na wanaitegemea ardhi hiyo katika kuzalisha zao hilo Moja tu.
“Mbegu ya tatu ni TARI SOR1 ni mbegu ambayo rangi yake ni kahawia Ina uwezo wa kuzaa tani 3 mpaka Tani 3.6 kwa Heka Moja,sifa yake nyingine ya ziada ni uwezo wake wa kukabiliana na gugu chawi kiduha kwa hiyo tinawashauri wakulima wanaotembelea maeneo haya watumie mbegu hizi I waweze kulima kwa tija,” amemaliza.