Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala wakiwasili katika hospital ya Wilaya ya Kusini Zanzibar kwa ajili ya kuwaona wagonjwa pamoja na kufanya usafi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Comred Mohamed Ramadhani Msofe akifanya usafi katika hospital ya Wilaya Kusini.
Mbunge wa Viti Maalamu Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Mwantumu Dau Haji akifanya usafi katika hospital ya Wilaya Kusini
Mbunge wa Viti Maalamu Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Mwantumu Dau Haji akitoa zawadi kwa Mama aliyejifungua katika hospital ya Wilaya Kusini.
Mbunge wa Viti Maalamu Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Mwantumu Dau Haji akiwa katika picha ya pamoja na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala baada ya Kutembelea Hospital Wilaya ya Kusini iliyopo Kijiji Cha Kitogan.
NA NOEL RUKANUGA, ZANZIBAR
Mbunge wa Viti Maalamu Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Mwantumu Dau Haji leo tarehe 18/7/2023 ameungana na Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala kutembelea wagonjwa na kusafisha mazingira katika Hospitali ya Wilaya ya Kusini Unguja kijiji cha Kitogani.
Akizungumza baada ya kumaliza kufanya usafi na kuwaona wagonjwa pamoja na watoto waliozaliwa Mhe. Mwantumu Dau Haji, amesema kuwa wanaendelea kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu ili watoto kuwaepusha na kila jambo baya katika maisha yao.
Amesisitiza umuhimu wa wazazi kuzingatia malezi ya watoto ili kuhakikisha wanakuwa na maadili mema katika jamii.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Comred Mohamed Ramadhani Msofe, amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu muhimu wa kuzingatia maadili mema katika jamii.
“Tumefanya usafi na kuwaona wagonjwa hii ni ibada kwetu tutaendelea kufanya matendo mema yenye kuleta tija katika Jumuiya yetu ya Wazazi” amesema Comred Msofe
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kusini Unguja Dkt. Rwanyumba Mlogasila ameishukuru ujio wa Jumuiya ya wazazi CCM Ialla kwa kuonesha upendo wa kuwaona wagonjwa pamoja na kufanya usafi.
“Mmetupa faraja watumishi wa hospital hii, hivyo tunawaadi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kujituma ili kuendana na kasi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” amesema Dkt. Mlogasila.