Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) , Bw.Rashid Mtima akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo mei 26,2022 katika Ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) , Bw.Rashid Mtima akizungumza na waandishi wa habari leo mei 26,2022 katika Ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) wamekanusha habari zilizotolewa na gazeti la Jamhuri Mei 10-16 tolea la 554 lililosomeka kuwa “Fedha za TALGWU zapigwa”.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 26,2022 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TALGWU, Bw.Rashid Mtima amesema katika gazeti hilo liliandika kiasi cha Bilioni 1.1 za kuchapa sare 80,000 kupigwa , taarifa hiyo si ya kweli kwani mapaka sasa mzabuni wao Savana General Merchandise amelipwa jumla ya 700,000,000 kwa mujibu wa mkataba na sio shilingi bilioni 1.1 kama ilivyoripotiwa,
Amesema Gazeti la Jamhuri liliripoti kwamba linataarifa kwamba Mzabuni Savana General Merchandise alitafutwa na mjumbe mmoja wa bodi ya zabuni huku akidaiwa uwezo wake wa mtaji kifedha ni mdogo na alilipwa huku sare hizo hazijafanyiwa uhakiki.
“Ieleweke kwamba TALGWU ina taratibu zake za kutafuta Mzabuni kwa mujibu wa kanuni za manunuzi za Chama toleo la 2018 kwa ajili ya zabuni zote ambazo kampuni au wazabuni huomba kwa kila mwaka na si kuletwa na kiongozi au mjumbe wa bodi ya zabuni kama inavyoelezwa na gazeti la Jamhuri”. Amesema Bw.Mtima.
Ameeleza kuwa mchakato wa manunuzi ya sare za Mei Mosi za mwaka 2022 ulizingatia taratibu zote za manunuzi kwa mujibu wa kanuni za manunuzi yya chama za mwaka 2018 na kitabu cha zabuni namba TTALG/PROC/0021/2021 na kupelekea kumpatia mzabuni Savana General Merchandise ambae alipewa kazi ya uchapishaji.
“Mzabuni alipewa kazi ya uchapaji na usambazaji wa sare 80,000 zenye thamani ya 1,196,000,000. Lakini baada ya mapokezi ya sare hizo ikagundulika kwamba kuna mapungufu makubwa ya ubora wa sare ikilinganishwa na makubaliano kwa mujibu wa mktaba”. Ameeleza
Pamoja na hayo TALGWU imewaasa waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia taaluma na maadili ya uandishi wa habari ili kuhakikisha kuwa wanaandika habari za ukweli na za kutokupotosha Umma na kuharibu taswira ya taasisi.