Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda, yakilenga kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, hususan katika sekta ya mafuta na gesi.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, ukiwa na umuhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo ya sekta ya nishati katika nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Marco Gaguti, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio, Kamishna wa Mafuta na Gesi, Bw. Goodluck Shirima, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame.