Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara,John Mongela mwenye (kofia ya kijani) akizungumza bara baada ya kufika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou toure Jijini mwanza
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou toure, Dkt. Bahati Msaki akisoma taarifa ya hosptali hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongela akizungumza na baadhi ya watumishi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Sekou toure pamoja na viongozi wa chama hicho pamoja na wanachama katika ukumbi wa Hosptali hiyo.
……………
Na Hellen Mtereko,
Mwanza
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Mongela amesema jamii ambayo ina afya njema ndiyo inaweza kushiriki vizuri katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo kuanzia kwenye ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.
Hayo ameyabainisha Leo Jumatano Februari 4, 2026 wakati alipotembelea na kukagua Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Sekou toure iliyoko Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya chama hicho.
Mongela ameeleza kuwa jamii ambayo inapata elimu bora na afya njema inaweza kupambana vizuri katika kukuza kipato.
Amesema dhamira kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ni kuendelea kuboresha sekta ya afya ili wananchi wazidi kupata huduma bora hatua itakayosaidia kuleta ustawi mzuri katika jamii.
Kwaupande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou toure, Dkt. Bahati Msaki amesema wanahudumia wagonjwa wa nje 450 hadi 500 kwa siku huku wagonjwa wanaolazwa kwa siku ni kati ya 50 – 60.
Aidha, amesema Hosptali ilipokea mashine ya CT -Scan kutoka Wizara ya afya kupitia mradi wa usambazaji vifaa tiba vya mionzi (ORIO) yenya thamani ya bilioni mbili.
“Uwepo wa mashine hii umeboresha huduma mbalimbali za uchunguzi ambapo kuanzia julai 2025 hadi Disemba 2025 jumla ya wagonjwa 934 wamepatiwa huduma za uchunguzi, uwepo wa mashine hii umepunguza idadi ya wagonjwa ambao walikuwa wanapewa rufaa kwenda kufanya kipimo katika Hosptali ya Kanda ya Bugando”, Amesema Dkt. Msaki
Amesema Hospitali hiyo ina mashine kumi za kutoa huduma ya kusafisha damu (Dialysis), huduma hiyo ilianza kutolewa Machi, 2022 ambapo jumla ya wagonjwa 101 wamenufaika na huduma hiyo na 11 wanaendelea na huduma hiyo hadi sasa.
Akizungumzia maboresho yanayoendelea katika Hosptali hiyo, Dkt. Msaki amesema wanategemea kuanza ujenzi wa jengo jipya la kisasa lenye thamani ya bilioni 22 ambalo litakuwa na ghorofa tisa na litahudumia wagonjwa wa dharura na ajali (EMD), OPD na wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU)
“Wizara ipo kwenye mpango wa kumtafuta mkandarasi kwa mwaka 2022/2023 hospitali iliingiziwa bilioni moja hivi sasa wizara ya afya inakamilisha taratibu za kumpata mkandarasi kwani mshauri mwelekezi tayari alishapatikana”,



