Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza uamuzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya Mikutano Mikuu ya Shirika hilo, ikieleza kuwa uamuzi huo ni mafanikio makubwa kwa Tanzania, Afrika na mamilioni ya wazungumzaji wa Kiswahili duniani.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 43 wa UNESCO unaofanyika jijini Samarkand, Uzbekistan Novemba 11, 2025, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye UNESCO Mhe. Ali Mwadini amesema hatua hiyo inatambua umuhimu wa lugha katika utambulisho, umoja na maendeleo.
Mhe. Balozi Mwadini amesema Serikali ya Tanzania itashirikiana na UNESCO kukuza Kiswahili
i kupitia tafiti, elimu na teknolojia za kidijiti, ikiamini kuwa lugha hiyo itazidi kuchangia amani, ushirikiano na maendeleo endelevu duniani.



