Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara yake kuelekea Miaka sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZBC Karume House Mnazi mmoja Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Soraga wakati akizungumza kuhusiana na Mafanikio ya Wizara yake kuelekea Miaka sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZBC Karume House Mnazi mmoja Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga akifafanua jambo wakati akijibu maswali alioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara yake kuelekea Miaka sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZBC Karume House Mnazi mmoja Zanzibar.

Muandishi wa Habari wa Idara Habari Maelezo Sheha Haji Sheha akiuliza maswali katika Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara yake kuelekea Miaka sitini ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZBC Karume House Mnazi mmoja Zanzibar.
NA SHEHA SHEHA, MAELEZO -12.12.2023
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema Serikali inalenga kuimarisha uwezeshaji wa Wananchi ili kuleta ustawi kiuchumi Nchini.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa Wizara hiyo kwa Waandishi wa Habari huko Karume House Mjini Unguja katika kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema Serikali ya awamu ya nane imeimarisha uratibu wa masuala ya Uwezeshaji kwa kutayarisha sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi ili kuweka usimamizi mzuri wa utekelezaji kwa Wananchi.
Amesema Wizara hiyo imefanya mazungumzo na Wawekezaji Nchini kwa lengo la kuweka namna bora ya kuwasaidia wananchi katika miradi yao ili dhamira ya Wananchi kunufaika na uwekezaji huo.
Vilevile amesema Serikali imeandaa Mfumo wa Taarifa za soko la Ajira ili kuzitambua fursa za ajira ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha Wananchi kuzitumia fursa hizo ili kupunguza idadi ya Vijana wasio na Ajira.
Aidha amesema Serikali ya awamu ya nane imeazimia kufanya Mageuzi ya Mfumo wa Vyama vya Ushirika ili viwe imara, endelevu, vinavyoendeshwa kiujasiriamali na vinavyokidhi mahitaji ya wanachama kiuchumi na kijamii.
Kwa upande mwengine, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Hussein Ali Mwinyi kwa kufuatilia kwa karibu utendaji wa taasisi za Serikali kupitia maagizo, maelekezo, ziara na majadiliano ya ana kwa ana na watendaji wa Serikali, Mfumo wa Sema na Rais (SNR- Mwinyi) pamoja na Taasisi ya Ufuatiliaji wa utekelezaji wa vipaumbele vya Mheshimiwa Rais (PDB) Hatua ambazo zimeweza kuimarisha ufanisi katika utendaji wa majukumu ya Wizara na taasisi za Serikali.



