Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya _Y & P Architect_, Mhandisi Yasin Mringo, akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, alipofika kwa ajili ya kusaini *Mkataba wa Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe ( Kampasi Kuu)* chini Mradi HEET. Hafla hiyo imefanyika tarehe 09.10.2023 viunga vya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu.
Mratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Eliza Mwakasangula, akitoa maneno ya utangulizi na kumkaribisha Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo ili kufungua hafla ya kusaini *Mkataba wa Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu*) chini ya Mradi HEET. Mkataba huo umesainiwa kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na kampuni ya _Y & P Architect_ leo tarehe 09/10/2023 katika viunga vya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu).
Mratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe upande wa Miundombinu Bw. Leonard Prosper, akielezea kwa kifupi shughuli zitakazotekelezwa na kampuni ya _Y & P Architect_ kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa wa *Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu)* chini ya Mradi HEET, katika hafla iliyofanyika tarehe 09/10/2023 katika viunga vya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu).
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akifungua hafla ya kuweka saini *Mkataba wa Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu)* kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na kampuni ya _Y & P Architect_. Hafla hiyo imefanyika tarehe 09/10/2023 Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu).
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (kulia) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa hafla ya kusaini *Mkataba wa Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu)* chini ya Mradi wa HEET. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya _Y & P Architect_ (iliyoshinda zabuni) Mhandisi Yasin Mringo. Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 09.10.2023 katika viunga vya Chuo Kikuu Mzumbe huku ikihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Menejimenti ya Chuo hicho.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya _Y & P Architect_, Mhandisi Yasin Mringo (kushoto) wakiwa wameshika nakala za *Mkataba wa Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu)* chini ya Mradi wa HEET baada ya pande zote mbili kusaini mkataba huo. Hafla hii ya utiaji wa saini mkataba tajwa imefanyika leo tarehe 09.10.2023.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Mipango, Fedha na Utawala) Prof. Allen Mushi, akitoa neno la shukrani baada ya kuhitimishwa kwa hafla ya kutia saini *Mkataba Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu)* chini ya Mradi wa HEET. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe na waratibu wa mradi wa HEET imefanyika leo 09/10/2023 chuoni hapo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya _Y & P Architect_ Mhandisi Yasin Mringo (kushoto) wakikabidhiana *Mkataba wa Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe (Kampasi Kuu)* chini ya Mradi wa HEET baada ya kusaini mkataba huo leo 09.10.2023 katika viunga vya chuoni hapo.

Menejimenti ya Chuo, Waratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya _Y & P Architect_, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya hafla ya kusaini *Mkataba wa Kutoa Huduma ya Ushauri wa Kitaalamu wa Usanifu na Usimamizi wa Miundombinu Mipya Chuo Kikuu Mzumbe, (Kampasi Kuu)* chini ya Mradi wa HEE leo tarehe 09.10.2023 katika viunga vya Chuo tajwa.



