Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Bw. Adam Fimbo akizungumza na vuombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania kuhusu maadhimisho ya miaka 20 na mafanikio ya taasisi hiyo Leo jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi wa dawa za binadamu na mifugo , Emmanuel Alphonce akiwasilisha mada kwa Waandishi wa Habari waliohudhulia katika kikao kazi hicho,Septemba 22.2023.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudencia Simwanza akiwasilisha mada ya Wajibu wa Waandishi wa Habari katika kulinda Afya ya Jamii, katika kikao kazi cha TMDA na Waandishi wa Habari,Septemba 22.2023.
Kaimu Meneja huduma za Sheria wa TMDA, Martha Malle akiwasilisha mada kwa Waandishi wa Habari waliohudhulia katika kikao kazi hicho, Septemba 22.2023.

Na Sophia Kingimali
Wakati wakiendelea kuazimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba (TMDA)Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Adam Fimbo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za madhara yanayotokana na dawa pindi wanapokutana na changamoto hiyo ili waichukue dawa hiyo sokoni na kuifanyia vipimo ili kuokoa wengine.
Wito huo ameutoa leo Septemba 22 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali nchini kuelezea mafanikio waliofanya kwa miaka 20 ya TMDA na kutambua mchango wa vyombo vya Habari katika kuelimisha umma.
Amesema dawa zinazotumika kutibu magonjwa mbalimbali zinaweza zikatibu au zisitibu na kuleta madhara kwa mtumiaji.
“Wito wetu kwa wananchi ni wao ndio wanatumia kila siku kwa ugonjwa ambao unakusumbua hivyo toa taarifa ukiona dawa fulani inakusumbua au unatumia haikupi matakoe ambayo yanatakiwa,”amesema Fimbo.
Amesema TMDA ina mifumo ambayo inasaidia wao kufahamu dawa kama inatibu au haitibu lakini kutokana na asili ya dawa hizi ni kemikali zikikaa muda fulani au kutegemeana na mwili wa binadamu uko dhaifu kiasi kiasi gani.
Amesema usajili wa dawa unasaidia kuhakiki au kudhibiti kwa sababu matoleo yanatengenezwa katika vipindi tofauti inawezekana ikatokea dawa ina shida fulani.
“Dawa jinsi zilivyo zina madhara kwa watumiaji nasisitiza kwa wananchi kama dawa unatumia inaleta madhara toa taarifa ili kufahamu dawa ina madhara kwa watu wa aina gani wazee, watoto wajawazito ili itusaidie kubaini madhara mapema na kuweza kuchukua hatua mapema ili athiri isitokee kwa walio wengi”.
Amesema hilio ni jukumu kubwa la TMDA kwani kuna dawa bandia na duni sokoni kwa sababu dawa hazina mipaka zinavuka ikitokea dawa una mashaka nayo unapaswa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika.
Aidha amesema TMDA ni taasisi ambayo inaongoza barani Afrika katika suala la mifumo na udhibiti wa dawa ukaguzi wa usajili, bidhaa na usalama wa dawa kwenye soko.
“Mifumo yote imefanyiwa uhakiki na Shirika la Afya Duniani (WHO) sasa hivi tunaongoza na wenzetu wa SADEC wamekuja kujifunza taratibu ziko je na tunafanya je kazi na tunatoa mafunzo, “amesema.
Amesema TMDA ni kivutio mahili kwa usajili wa dawa barani Afrika na utoaji huduma maabara zao zinafanya uchunguzi wa kisayansi na mambo mengine mengi.
Aidha Fimbo amesema kushirikiana na waandishi wa habari na wahariri wameona umuhimu kwa kazi wanazofanya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu TMDA na kulinda afya za jamii.
Wakati huo huo Mkurugenzi huyo alitoa tuzo kwa waandishi wa habari waliofanya habari za kuelimisha jamii kuhusu TMDA amesema zoezi hilo ni endelevu ili kuendelea kuhamasisha waandishi wa habari kuzidi kutoa elimu kwa umma.
Naye Mkurugenzi Mdhibiti wa Dawa Vifaa Tiba na Vitendanishi wa TMDA, Kissa Mwamita amesema ametoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusiana na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili wao wakaelimishe jamii.
Amesema madhara yatokanayo na vifaa vya afya kuna mifumo ambayo mwananchi akitumia dawa au vitendanishi watoe taarifa TMDA ili waweze kufanya tathimini.
“Mtengenezaji dawa yeyote ana ainisha madhara ambayo yanaweza yakampata mtumiaji na kitu cha kawaida kabisa mamlaka kufuatilia kwa ukubwa gani madhara yanawapata wananchi, “amesema Kissa.
Amesema kupatikana kwa madhara pia kuna sababishwa na hali tofauti inawezekana ikawa ni ugonjwa au mchanganyiko na dawa nyingine
“Taarifa tunazozipokea wakati wa kufanya tathmini unakuta wengi wanapata madhara ambayo tayari mtengenezaji aliyaanisha kuwa yanapatikana ukitumia dawa hizi,” amesema.
Amesema mara chache sana mtumiaji kupata madhara ambayo yapo nje ya yale aliyoainisha na mtengenezaji kwa watu 200 unaweza kuta ni mmoja ndie aliepata madhara.
Aidha amesema dawa ,vifaa tiba na vitendanishi zilizopo nchini ni salama mamlaka ipo makini katika kuhakikisha wanafuatilia kuanzia dawa zinapoingizwa hadi zitakavyotumika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Huduma ya Maabara TMDA, Dk. Dastan Hipolite amesema maabara ya mamlaka imeendelea kupokea sampuli ambapo mpaka sasa wamepokea sampuli 1372 za dawa kwa mwaka tangu 2006 hadi 2023.
“Serikali imefanya uwekezaji mkubwa Sana katika maabara ikiwemo vifaa vya kisasa vya upimaji sampuli mashine na mpaka nchi za jirani wanakuja kujifunza hapa na kuleta sampuli zao hapa wanalipia na serikali inapata pato,”amesema Dk. Hipolite.



