Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amechangia kiasi cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya kuboresha huduma katika Kanisa katoriki la parokia ya Tumbi lililopo katika Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Mhe.Koka amechangia fedha hizo wakati wa ibada ya kubariki ndoa ya Katibu wake Method Mselewa iliyofanyika katika Kanisa Hilo mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa serikali,vyama vya siasa pamoja na viongozi wa dini.
Koka alisema kwamba ameamua kuchangia fedha hizo ambazo zitaweza kusaidia katika kununua mabenchi kwa ajili ya kukalia waumini kiasi cha milioni mbili na shilingi milioni moja zitakweñda kutumika kwa ajili ya wana kwaya wa Kanisa hilo la Tumbi.
“Kimsingi mm pamoja na mke wangu leo tumejumuika hapa lkn kwa ajili ya kushuhudia ndoa ya msaidizi wangu Method kwa kweli nimefàrijika sana na pia tumekuja kwa ajili ya kumuomba Mungu kwa hiyo mm nachangia milioni tatu kwa ajili ya Kanisa letu kwani hapo awali alikuwa hivi linazidi kuwa na mahitaji mbali mbali,”alisema Koka.
Mbunge Koka alibainisha kuwa ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi pamoja na waumini wa kanisa hilo kuendelea kusaidia kwa hali na mali katikà mambo mbali mbali ikiwemo.huduma na mahitaji mengine ya msingi.
Kwa upande wake mke wa Mbunge Selina Koka ambaye na yeye alihudhuria katika ibada ya ndoa hiyo ya Medhod aliahidi kuendelea kushirikiana na parokia hiyo pamoja na waumini wote katika kuboresha zaidi kanisa hilo.
Kwa upande wake Padri wa kanisa hilo ambaye ndiye aliyebariki ndoa hiyoTasilo Nchimbi alimshukuru kwa dhati Mbunge Koka pamoja na mkewe Selina kwa kuwa na moyo wa upendo na kujitolea katika kulisaidia kanisa katika mambo mbali mbali ya msingi ikiwemo kuchangia fedha hizo milioni tatu.
Padri Tasilo alisema Koka amebarikiwa na mwenyezi Mungu kutokana na kuwa karibu na wananchi na kulisaidia kanisa ununuzi wa mabenchi ikiwa sambamba na kuona umuhimu wa kuwajari na kuwathamini waimba kwaya kwa ujumla na kuwachangia milioni moja.
Nao baadhi ya waumini wa kanisa hilo ambao pia ni wana kwaya hawakusita kumshukuru Mbunge huyo kwa majitoleo yake kutoka moyoni kwa dhamira kubwa ya kuisaidia kwaya pamoja na kulisaidia kanisa hilo la Tumbi katika ununuzi wa mabenchi ya kukalia.