Na Sophia Kingimali
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya mifumo ya chakula (AGRA) na kampuni ya John Deer inatarajia kuanza mchakato wa kuwashindanisha vijana kwenye vikundi na kuwapatia zawadi ya trekta lengo likiwa kuendelea kuhamasisha vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo.
Hayo ameyasema Leo September 8 jijini Dar es salaam na Waziri wa Kilimo Hissein Bashe katika siku ya mwisho ya mkutano wa Mifumo ya chakula Afrika AGRF wakati akikabidhiwa trekta Hilo waziri wa kilimo kilimo Hussein Bashe.
Amesema mchakato ikianza vijana watapaswa kuiandaa andiko la wazo la kilimo wanachotaka kukifanya na kikundi kitakachoshinda watakabidhiwa trekta hiyo.
“Tutatangaza mashindano vijana wataleta maandiko watakaoshindana, wazo lao la biashara na namna ya kufanya biashara katika shughuli za uzalishaji Mkakati huo wa kupata mshindi utakuwa wa wazi”amesema Bashe,
Amesema Kikundi kitakachoshinda kitakabidhiwa trekta Ili kuangalia namna vijana watakavyoenda kufanya kazi za kibiashara katika kilimo.
Amesema Mwelekeo wa serikali ni kujaribu kutafuta mbinu za kiwaingiza vijana katika kilimo,
“sio kila kijana atakuwa na shamba, kunamwingine atalima, mwingine atauza mbegu mwingine atatoa huduma za ugani.”amesema Bashe
Akizungumzia upatikanaji wa mbegu Bora za mazao ya chakula nchini amesema bilioni 650 zinahitajika ili kuhakikisha mbegu hizo zinazalishwa nchini
Amesema Sekta binafsi ilizindua mbegu ya kitanzania 2021 huku uwezo wetu wa kuzalisha mbegu ndani ya nchi ulikuwa asilimia 20 ya mahitaji,
“mahitaji yetu ya mbegu kwa mwaka huu wa kilimo yalikuwa tani laki moja na elfu ishirini”amesema
Aidha ameongeza kuwa Watanzania ndani ya nchi wamezalisha tani elfu 60 ambayo sawa na asilimia 50, ya mahitaji
Amesema njia iliyoweza kuongeza uzalishaji ni njia mbili ikiwepo makadirio ya mahitaji na mahitaji halisi.
Makadirio ya mahitaji kwenye kilimo ni makubwa sana lakini mahitaji halisi ni tani laki moja na elfu ishirini ya mbegu za mazao yote.
“Tumeweza kufika asilimia 50 ya uzalishaji serikali inaendelea kuwekeza kwenye mashamba umma, mwaka jana tumeanza kujenga miundombinu ya umwagiliaji na si muda mrefu tutazindua mashamba ya serikali yaliyowekewa miundombinu ya umwagiliaji ya kisasa ambayo yatatumika kwaajili ya uzalishaji wa mbegu.”ameongeza Bashe,
Amesema katika mashamba 17 ya serikali atakayezalisha katika hayo mashamba sio serikali ni sekta binafsi ya ambazo zitakua zinajihusisha na uzalishaji wa mbegu.
Amesema serikali imeweke nguvu kwenye utafiti ili kuweza kuleta mbinu bora za kilimo cha kisasa, na waweze kuwapa sekta binafsi waweze kuzalisha kwa wingi.
Amesema maelekezo ya Rais ndio welekeo serikali ifikapo 2025 asilimia 75 za mbegu Bora na mazoa ya chakula zizalishwe nchini na si kuagiza kutoka nje.



