Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) pamoja na Waumini wa Kanisa hilo, kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023
….
Julieth Laizer, Arusha .
Arusha .RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kuwa , kuhusu utekelezaji wa mkataba wa bandari wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai ameamua kunyamaza kimya na ataendelea kunyamaza kimya kwani hakuna mwenye misuli na ubavu  wa  kuligawa Taifa hili.
Ameyasema hayo leo agosti 21 jijini Arusha katika maadhimisho ya miaka 60 ya KKKT katika Chuo kikuu cha Tumaini Makumira mkoni Arusha .
“Nimeyasikia yote  uliyoyasema (Askofu Shoo) kuhusu usalama ,amani,umoja na mwendelezo wa Taifa letu,niliamua kunyamaza  kimya na ninaendelea kunyamaza kimya. 
“Ninachotaka kuwahakikishia ni kuwa hakuna mwenye misuli  na ubavu wa kuligawa Taifa hili,hakuna mwenye misuli  na ubavu wa  kuharibu wala kuuza Taifa hili.”amesema Rais Samia.
Amesema  ,viongozi wa dini ndio wenye jukumu la kukuza kusimamia na kutunza maadili yetu kama watanzania ili vijana wetu waishi  maisha ya kumpendeza  Mungu ,tuwakuze watoto  wetu waishi maisha ya kumpendeza Mungu naomba viongozi wa dini wabebe  jukumu hili  kwa kiwango kikubwa.”amesema. 
Samia amesema ameshuhudia namna ambavyo  kanisa hilo wamekuwa   wakitoa huduma mbalimbali za kiroho  na kimwili kwa zaidi ya  miaka 60  na leo ni maadhimisho ya kitaifa kwa kanisa hili ni jambo kubwa sana la kumshukuru  Mungu.
Ameongeza,Serikali imekuwa ikishirikiana na Taasisi za kidini  katika kutimiza wajibu wake ndo maana wote kwa pamoja wamekuwa wakishirikiana  katika kuchangia maendeleo ya nchi 
 “Nawaahidi kuwa,Taasisi za dini zote serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zote zinazowakabili kwa ustawi wa maendeleo  ya nchi yetu “.
Ameongeza ,kila mmoja wetu ni shuhuda kwa namna ya mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyotokea  kwa watu wa vizazi vyetu na hii ni kutokana na kuwa   tumeacha kutunza dunia na kufanya mabaya,hivyo kuwataka kubadilika na kuyatunza mazingira yetu kwa manufaa ya nchi yetu kwa ujumla.
“Mazingira  hayaachi kutuadhibu kama tunavyoyaharibu  sisi naomba wote tukawe  rafiki wa mazingira  kwani uhifadhi wa mazingira  ni jukumu letu sote na nawaomba sana Wananchi watumie vyanzo mbadala katika kukabiliana na mabadiliko  hayo ya tabia ya nchi  .”amesema Rais Samia.
Aidha amewataka wenye  kanisa kujidhatiti kuendana na yale mabadiliko, huku akiwataka viongozi wa dini kudumisha umoja na sala ili nchi iweze kuishi kwa amani. 
Amewapongeza kwa dhati viongozi waliomaliza nafasi zao na kuwaomba viongozi watakaochaguliwa  kuendeleza misingi  mizuri  ya kanisa.
Naye Askofu Mkuu wa kanisa la KKKT ,Frederick Shoo amesema kuwa ,wao kama kanisani wanaunga mkono swala la uwekezaji katika Dp World   na ya kuwa wao hawapingi uwekezaji kwani wanajua serikali inahitaji wawekezaji. 
“Mheshimiwa Rais unakumbuka sisi viongozi wa dini  tulikuomba kuja kuonana na wewe  madhehebu yote  ya kikristo ulitusikiliza na kupokea maoni yote na kuahidi kufanyia kazi kwa maslahi mapana ya Taifa. 
“Tunakuamini  katika jambo hili Mheshimiwa   kuwa taasisi na vyombo vyake vitafanyia kazi jambo hili tena kwa umakini mkubwa .”amesema Askofu Shoo.
Askofu Shoo amesema , kupitia jambo hili kuna watu wanataka kugawanyika kabisa kwa sababu zao lakini wanamshukuru Mungu kama mama na kiongozi amekaa kimya,na jambo hili linahitaji  umakini katika kuliendea jambo  hili  pasipo nchi kugawanyika. 
“Kanisa lipo pamoja na tutaendelea kukuombea  na kanisa litaendelea kuunga  mkono kwa maslahi ya Taifa letu. “.
Kanisa litaendelea kusimamia haki za binadamu na kuheshimu  mamlaka zilizopo jambo ambalo litaimarisha umoja wa kimataifa kwani kazi yetu kubwa ni kuwaombea kuhakikisha kila kitu  kinaendea  sawa.
“Hata tukipata sehemu ya kukemea  tutakemea pia ila tunaomba tusiambiwe  tunachanganya dini  na siasa. “
Aidha Shoo amewataka Viongozi wa dini kutumia  nafasi zao kulizungumzia swala la mabadiliko ya tabia ya nchi ili kunusuru  nchi yetu huku akiwataka kujiingiza  kwenye maswala ya nishati mbadala.
“Viongozi  wenzangu  na wanasiasa tuache kuwagawa watu kwa misingi ya kisiasa  na kwa maslahi  binafsi ,anayefanya hivyo kwa nia mabovu akemewe na asionewe  aibu  kabisa, na  kanisa lipo tayari kuwa na serikali katika maswala mbalimbali .”.
 
Amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo mwaka 1963 walikuwa na waumini laki  5  ambapo kwa sasa  wapo waumini milioni 8 na wana dayosisi 27 sasa na zingine zinaendelea kuzaliwa. 
Amesema kanisa hilo  limeenea katika mikoa yote ya Tanzania bara  na tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo
 limekuwa likitoa  huduma za jamii katika kuhudumia kimwili  na kiakili. 
Ameongeza kuwa ,kumekuwepo na ushirikiano  wa kutosha kwenye maswala ya elimu kwa kuwepo kwa shule zenye vipaji  maalumu ambapo kanisa limetoa  kwa serikali .
“Mimi nilikereka juzi kusikia mtu anasema  kwa nini serikali inatumia fedha zake kusaidia Taasisi za dini na hiyo tunaweza kusema huyo mtu hajui historia  ila ana sababu zake nyingine.”amesema .
Fedha zinazotokana  na kusamehewa  kwa taasisi hizo fedha hizo zishirikiane kuendelea kuchangia maendeleo  na serikali  kwani kuna baadhi ya wanasisiaa wanapiga  vita  swala hilo nafikiri  ni vizuri tukaheshimu ushirikiano huo na asiwepo mtu yoyote wa kubeza  ushirikiano  huo katika ya serikali na taasisi hizo.
“Mheshimiwa Rais nakupongeza sana kwa kushika nchi na mimi nasema huu ulikuwa ni mpango rasmi wa Mungu nakuomba Mheshimiwa Rais ufanye kazi yako kwani Mungu ndo kakuweka  kwenye  nafasi hiyo na sisi tunaheshimu hilo watu ambao hawajaridhika   na uwepo wako hadi sasa nawapa pole sana”
Amesema kuwa,uwepo wa mshikamano kwa wananchi wote katika kukuza uchumi wa demokrasia na uhuru wa kuongea,napongeza sana falsafa  yako ya kukuza uchumi.