Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. Nicodemus Mushi Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA wakati alipotembelea kwenye banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipokea zawadi kutoka kwa Bw. Nicodemus Mushi Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA wakati alipotembelea kwenye banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiwasili katika banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA alipotembelea kwenye banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.
………………………………
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa wanatambua kazi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kutoa huduma za usafirishaji wa upokeaji wa mizigo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la TPA katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Amesema kuwa katika mipango ya Bandari ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi katika kuongeza uwezo zaidi katika utoaji wa huduma.
Amesema kuwa katika kipindi hiki kuwepo sekta binafsi itasaidia kusukuma mbele sekta ya kilimo kwa kusafirisha mazao mbalimbali yanayozalishwa na wakulima wa ndani na wale wawekezaji katika sekta hiyo.
Aidha amesema kuwa serikali iko bega kwa bega katika kuhakikisha bandari inakwenda katika kuendelea kuongeza mapato na uchumi wa nchi.
Kwa Upande Bw. Nicodemus Mushi Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA amesema kuwa TPA imeweza kuongeza miundombinu ya kisasa katika kuhudumia meli zinazoingia nchini.
Amesema katika hatua nyingine wanatarajia kujenga miundombinu kwa ajili ya mazao yatayokuwa yanasafirishwa nje ya nchi .