Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka Wafanyabiashara wadogo Wamachinga, Mama Lishe , Madereva wa bodaboda na Bajaji waendelee kufanya vikao vya mara Kwa mara ili kupunguza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Chalamila ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika Mkutano uliowakutanisha Wafanya biashara hao Kwa lengo la kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utendaji kazi wake ambapo amesema wanatakiwa wawathamini Kama Wafanyakazi wengine Kwa kuwatatulia changamoto zao
Hata hivyo amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala Eduward Mpogolo na Timu yake Kwa kuwathamini Wafanya biashara hao na kuongeza kuwa hatazikataza pikipiki na Bajaji kuingia Mjini kwani wanatakiwa wazingatie tararibu na Sheria za Usalama barabarani
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewahakikishia Wafanya biashara hao kuwa watawaweka katika utararibu mzuri wa kuwawezesha kufanya kazi zao sambamba na kuwalinda.