Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Mji Amina Seif akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani  ikwemo serikiali kutoa fedha za kujenga sekondari mpya kupitia prorgam ya SEQUIP,,kushoto aliyekaa ni Mwenye kiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mheshimiwa Kelvin Mapunda

Mradi wa ujenzi wa sekondari mpya ya  Kata ya Lusonga katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambapo seriikali kupitia program ya SEQUIP imetoa zaidi ya shilingi milioni 560 kutekeleza sekondari hiyo ambayo imeanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu

baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Kata ya Lusonga mjini Mbinga wakiwa wameanza masomo yao mapema mwaka huu

Na Albano Midelo,Mbinga

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Imetoa zaidi ya shilingi milioni 560 kupitia program ya Uboreshaji Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kujenga sekondari mpya wilayani Mbinga.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Amina Seif amesema sekondari hiyo mpya inajengwa katika Kata ya Matarawe ambapo ujenzi wake utahusisha vyumba vinne vya madarasa,ofisi moja ya walimu,jengo la utawala,maabara tatu, maktaba, chumba cha TEHAMA,vyoo,kichomeaa taka na tanki la maji.

Hata hivyo Seif  amebainisha kuwa Halmashauri hiyo  hivi karibuni imepokea jumla  Shilingi Milioni 655,552,827.00 kati ya fedha hizo  shilingi 560,552,827 ni kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya ya kata ya Matarawe na shilingi milioni 95 ni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba  ya mwalimu ya familia mbili katika sekondari ya Lusonga.

 “Kwa niaba ya wananchi wa Mbinga,namshukuru   Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuletea fedha za kuboresha miundombinu ya elimu katika Halmashauri yetu hali ambayo itasaidia kuboresha elimu ya awali,msingi na sekondari’’,alisema.

Ameahidi kusimamia matumizi ya  fedha hizo  na kuhakikisha mradi wa ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu unakamilika kabla ya Oktoba 30,2023.

Serikali kupitia program ya SEQUIP katika wilaya Mbinga imetoa zaidi ya shilingi bilioni 1.8  kujenga shule mpya za sekondari katika kata za Lusonga,Amanimakoro na Matarawe.