Home Mchanganyiko TFCG, MJUMITA WAOMBWA KUSHIRIKI KAMPENI KUELIMISHA JAMII UTUNZAJI WA MISITU YA TAIFA

TFCG, MJUMITA WAOMBWA KUSHIRIKI KAMPENI KUELIMISHA JAMII UTUNZAJI WA MISITU YA TAIFA

0
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Fatma Mwassa akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya  Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) na waandishi wa habari za uhifadhi wa misitu wakati walipomtembelea ofisini kwake mkoani Morogoro Novemba 24,2022.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Fatma Mwassa akifafanua jambo wakati  akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya  Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) na waandishi wa habari za uhifadhi wa misitu wakati walipomtembelea ofisini kwake mkoani Morogoro Novemba 24,2022.
Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG  kulia na Elida Fundi Afisa Sera na Majadiliano Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu MJUMITA wakimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Fatma Mwassa mara baada ya kumaliza naye mazungumzo yao.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bi. Fatma Mwassa wakati akizungumza nao ofisini kwake mkoani Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Fatma Mwassa akiwa katika picha ya pamoja na Bettie Luwuge Afisa Mawasiliano wa shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania TFCG  kulia na Elida Fundi Afisa Sera na Majadiliano Mtandao wa jamii wa usimamizi wa Misitu MJUMITA.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Fatma Mwassa ameyaomba mashirika ya  Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kusaidia kutoa elimu ya uhifadhi wa misitu ya taifa inayosimamiwa na TFS  kutokana na uwezo ambao mashirika hayo yameonesha Katika kuhamasisha na kuelimisha jamii na wananchi kwenye  vijiji vya mfano vya wilaya za Mvomero, Kilosa na Mrorogoro DC katika kutunza misitu yao kutokana na Usimamizi mzuri wa mradi wa Mkaa Endelevu kwenye vijiji vyao.
Mkuu wa mkoa amezungumza hayo wakati alipokutana na timu ya waandishi wa habari za uhifadhi wa misitu na mazingira pamoja na maofisa wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) waliotembelea ofisini kwake Leo Alhamisi 24, 2022 ili kupata baraka zake na kumweleza malengo ya mradi huo ambao kwa sasa unaelekea ukingoni mwa utekelezaji wake.
Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa pamoja yalikuwa yakisimamia mradi wa mkaa Endelevu katika vijiji vya mfano kwenye wilaya za Mvomero, Morogoro DC na Kilosa mkoani humo ambapo wananchi wameelimika na kuhamasika namna ya utunzaji misitu ya asili katika vijiji vyao huku wakitengeneza Mkaa Endelevu kwa utaratibu maalum na wa kitaalam ambao umenufaisha vijiji vyao kwa miradi ya maendeleo pamoja na kipato cha mwananchi mmojammoja kutokana na mauzo ya Mkaa Endelevu.
Akifafanua zaidi mkuu wa Mkoa huyo ametoa tahadhari kwa  wakazi wa Morogoro kuhakikisha kabla hawajajenga katika maeneo yao wakachukue hati katika Halmashauri husika Ili waweze kupatiwa hati ya kumiliki ardhi na kibali cha Ujenzi ili kuepukana na changamoto za mbeleni.
Pia amewataka kutojenga katika maeneo ya hifadhi,maeneo ya milimani pamoja na kukata miti hovyo kwani miti ni uhai na ndiyo inaleta Mvua Nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa wakati akizungumza na waandishi wa habari sambamba na wadau wa Shirika la kuhifadhi misitu ya asili pamoja na Mjumita ambao wanaunga mkono juhudi za serikali katika Uhifadhi wa mazingira na misitu ya asili.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa uharibifu wa Mazingira Nchini huchangiwa na ukataji wa miti kwa shughuli za Binadamu,uchomaji wa mkaa,watu wanaochoma moto kusafisha mashamba na wimbi kubwa mifugo.
‘Kwa upande wa ukataji miti mara nyingi huwa inakuwa na kibali mara nyingine watu wanafanya kiuhalifu hivyo tunataka kuzuia vyote kwa sababu hatuna misitu kwa hiyo tumekaa na Wizara ya Maliasili na Utalii tuone tunatoa kipindi kumalizia leseni zilizopo na baada ya hapo tujipe muda wa kutafakari na kupanda miti badala ya kutoa vibali vya kuchoma mikaa n.k’amesema Mwasa
Aidha amesema kuwa ni vyema jamii ikatumia njia mbadala kutumia gesi kuliko kutumia mkaa kwani ili upate unateketeza tani saba za miti jambo ambalo linasababisha uharibifu wa mazingira.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa wamepewa maagizo kumi na Makamu wa Rais hivyo kila Wilaya imetengeneza mkakati wake wa utekeleza maagizo hayo ikiwa ni pamoja na kutokumili chenso ili kuepusha kukata miti hovyo.
Kuhusu changamoto ambayo wameibanini ni pamoja na rushwa kukithiri katika baadhi ya maeneo ikitokea wakati mtu amekamatwa na kuachiwa anapotoa rushwa.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Mwasa ameendelea kusema kuwa wameamua kuweka mipango mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na watu wanaharibu mazingira na pindi mtu atakapobainika watamchukulia sheria kali.
‘Ni aibu kwa taifa ni aibu kwa nchi kubwa kama Tanzania yenye miti mingi na misitu kufikia hatua hii mpaka hamna pa kushika na ukiingia katika misitu hiyo utaona jinsi imekatwa na watu jambo ambalo sio lizuri’ameendele kusisitiza Mwasa
Mkuu huyo wa mkoa ametoa rai kwa wnanachi kuepuka kuyaharibu mazingira kwa kukata miti hovyo badala yake wayatunze kwani kufanya hivyo kutasaidia kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi wa Usimamizi shirikishi wa Misitu ya jamiii(USMJ)  ulikuwa unatekelezwa chini ya Mradi wa Kuhifadhi Misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya Misitu (CoForEST) kwa ufadhili wa Shirika la  Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC).