Mkurugenzi  wa shule ya Fikiria kwanza iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha,Necta Lema akiwaasa wahitimu wa  kidato cha nne katika mahafali hayo shuleni hapo. 

Aliyekuwa mwenezi wa Meru  Joshua Mbwana (Mwarabu)akimkabiti cheti cha kuhitimu kidato cha nne mwanafunzi wa shule ya sekondari Fikiria kwanza iliyopo wilayani  Arumeru mkoani Arusha.

Meneja wa shule ya Fikiria kwanza ,Stephen Semfukwe akizungumza na wahitimu  pamoja na wazazi katika mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo. 
……………………..
Julieth Laizer,Arusha 

Arusha.Wazazi na walezi wametakiwa kushirikiana na walimu mashuleni  katika kusimamia maadili ya watoto wao  ili  kupata kizazi kilicho bora na salama. 

Hayo yamesemwa jijini Arusha na aliyekuwa Mwenezi wa  Meru (Mwarabu),Joshua Mbwana wakati akizungumza  katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya mchepuo  wa kiingireza  ya Fikiria kwanza iliyopo eneo la USA river wilayani Arumeru ambapo jumla ya wanafunzi 55 walihitimu .
 Mbwana amesema kuwa, swala la kulea  watoto  katika maadili ni la  wazazi wote kwa ujumla huku wakishirikiana na walimu ili kuweza kupata wanafunzi walio bora  na wenye maadili mazuri. 
Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanawapa  watoto  wao mahitaji yote wanayohitaji ili kuepukana na kujiunga na makundi yasiyofaa ambayo mwisho wa siku  hukatiza ndoto zao .
“Nawaombeni sana wazazi muwe  karibu na watoto wenu  msiwape uhuru  uliopitiliza kwani  kwa kufanya hivyo mtawapoteza hakikisheni  mnawalea  katika maadili mazuri na yenye kupendeza  ili waweze kuzifikia  ndoto zao walizojiwekea.”amesema Mmbwana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa  shule hiyo ,Necta Lema amesema kuwa,wamekuwa wakiwafundisha  watoto katika maadili mazuri sambamba na kuwaandaa kuweza kujiajiri kwa kuwafundisha stadi za kazi .
Aidha amewataka wazazi  wote kwa ujumla kuwajibika katika kupeleka  watoto shuleni ili wapate elimu iliyo bora sambamba na kuwalipia ada kwa wakati ili  waweze kutimiza malengo yao  waliyojiwekea. 
Aidha ameongeza kuwa,ni wakati sasa wa wazazi kujitahidi kuwalea  na kuwaongoza watoto wao  katika maadili  mazuri ili  wajiepushe na makundi mbaya huku akiwataka wahitimu kushika sana elimu kwani huo ndio uridhi pekee walioachiwa. 
Naye Meneja wa  shule hiyo ,Stephen Semfukwe amesema kuwa,wamekuwa wakifanya vizuri sana kitaaluma shuleni hapo ambapo  wamekuwa karibu na wanafunzi katika kuhakikisha  kila mmoja anafikia malengo  yao kwa kuendeleza vipaji vya watoto hao. 
“Katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wanarudi majumbani baada ya kuhitimu nawaombeni  sana wazazi mjitahidi kuwa karibu na watoto wenu sambamba na kuwafundisha kazi za mikono ili waweze kujiajiri  wakiwa tangu wadogo na kuondokana na changamoto  mbalimbali.”amesema Meneja .
Aidha amewataka wanafunzi hao kuongeza bidii ya kusoma zaidi na kuondokana na makundi yasiyofaa ambayo mwisho wa  siku yatawaharibia  maisha na kushindwa  kufikia malengo yao waliyojiwekea.
Baadhi ya wahitimu shuleni hapo, Diana Mmari na Martin Francis wamesema kuwa, wanashukuru kwa namna shule hiyo ilivyowaandaa kitaaluma na katika maadili mazuri na wanaahidi kufanya vizuri katika mitihani  yao na kuing’arisha shule hiyo kwa kiwango cha juu.