
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkoa wa Pwani kwa sasa una zaidi ya viwanda 1,460 ambapo kati ya hivyo 90 ni vikubwa na kila siku idadi inaongezeka.
Kutokana na kujipambazua na muitiko mkubwa kwa wawekezaji, Mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge ,amewaasa wawekezaji ndani na nje ya nchi waendelee kwenda kuwekeza na kujenga viwanda mbalimbali,kwani mkoa upo salama na kwenye Mazingira bora ya uwekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani hapo kuhusiana na wiki ya biashara na uwekezaji Kunenge alieleza mkoa wa Pwani una fursa nyingi katika utalii, biashara,viwanda,kilimo,ufugaji, Uvuvi.
Aliwakaribisha wawekezaji na kuwaeleza kuwa Mkoa wa Pwani ni Mahali sahihi kwa Uwekezaji Nchini kwani umesheheni maeneo ya kutosha yaliyotengwa kwa ajili ya kuwekeza na viwanda pamoja na miundombinu iliyo rafiki kwa ajili Yao.
“Pia upo Eneo la Kimkakati kwa Uwekezaji ikiwemo ukaribu Jiji la Dar es salaam, Uwepo wa Miundombinu muhimu kwa Uwekezaji ikiwemo Reli ya kisasa ya Mwendokasi SGR, Umeme na Maji kutosha na uwepo Kongani kubwa ya Viwanda Baran Afrika ya Sino Tan Kwala Industrial Park INAYOJENGWA viwanda vingi .”alisisitiza Kunenge.
Akizungumzia suala la TIN number ili kuongeza mapato ya mkoa alisema ,kwasasa wanadhibiti wenye viwanda Kuwa na Namba hizo mkoa wa Dar es salaam ambapo awali walikuwa wakinufaisha mkoa mwingine wakati wakiwa wamewekeza Mkoani hapo.
“Tuna Taasisi 17 ambazo tunashirikiana nao kusikiliza kero za wawekezaji na kuboresha Mji wetu,Nimeseme tuu katika maongezi yetu yanazaa matunda wengi wanalipa na kufanya usajili Mkoani kwetu, ngazi ya mkoa tunalifanyia kazi na linaleta tija ,”alisema Kunenge.
Hata hivyo ,alisema kwasasa wanapanga Maeneo mbalimbali ya mkoa Kuwa Mji wa kisasa ikiwemo Mji wa Kwala ,kupanga kisiwa cha Mafia ,suala hili ni la muda na michakato inaendelea.
Kufuatia mkoa huo kujinasibu na kuwa ukanda wa Viwanda ,unatarajia kuwa na wiki ya Biashara na Uwekezaji octoba 5-10 mwaka huu ,ikiwa ni maonyesho ya tatu tangu kuanzishwa kwa maonyesho hayo mwaka 2018, ambapo wanashirikiana mkoa ,Shirika linalohudumia Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) na kuratibiwa na TANTRADE.