
Dkt. Ladslaus Chang’a Mkurugenzi wa Masuala ya Utafiti na Matumizi hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA akizungumza na waandishi wa habari Katika maonesho ya Nanenane 2022 yaliyomalizika Leo kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

Dkt. Ladslaus Chang’a Mkurugenzi wa Masuala ya Utafiti na Matumizi hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA akitoa maelezo wakati akizungumza na waandishi wa habari Katika maonesho ya Nanenane 2022 yaliyomalizika Leo kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

Dkt. Ladslaus Chang’a Mkurugenzi wa Masuala ya Utafiti na Matumizi hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA akifaganua jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari Katika maonesho ya Nanenane 2022 yaliyomalizika Leo kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA imetoa ipo katika utekelezaji wa sheria ya namba 2 ya mwaka 2009 ambayo inamtaka kila mdau anayemiliki au wanaomiliki na kuendesha vituo vya utabiri wa hali ya hewa kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu kwa kusajili vituo hivyo ili kuviendesha.
Hayo yameelezwa na Dkt. Ladslaus Chang’a Mkurugenzi wa Masuala ya Utafiti na Matumizi hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA alipozungumza na waandishi wa hari katima maonesho ya kilimio ya Nanenane 2022 yaliyofungwa leo kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Dkt. Chang’a ametoa wito kwa wamiliki wote kufannya hivyo kwa kutii sheria na taratibu zilizowekwa ili kuepuka kuingia kwenye mkono wa sheria pale watakapobainika kuendesha vituo hivyo bila kufuata sheria na taratibu.
Ameongeza kuwa Maonesho ya Nanenane yamekuja katika wakati muafaka wakatiambapodunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ajenda ya mwaka huu 2022 “Kilimo ni biashara 20/30” kwamba ifikapo mwaka 2030 kama taifa katika kilimo liweze kuchangia angalau asilimia 10 ya pato la taifa.
Amesisitiza kuwa ili kufanikisha hayo kama watanzania tunapaswa kuzingatia huduma za hali yahewa kila mwananchi ambaye anatusikiliza anaalikwa na kusisitizwa kuhusu matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika mipango yake na kuzingatia sheria ya hali ya hewa ya mwaka 2009 ambayo imewekwa na serikali ili kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinaleta tija na ufanisi katika mipango yetu na katika maendeleo kwa ujumla.
” Nitoe Wito kwa wananchi kufutailia maelekezo na tabiri zote zinazotolewa hasa ukizingatia kwamba kuna changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo inaendelea kujikita katika kuathiri shughuli za maendeleo ikiwemo shughuli za kilimo,” Amesema Dkt. Ladslaus Chang’a
Amebainisha kwamba Mabadiliko ya hali ya hewa yanajitokeza wazi zaidi katika kuongezeka kwa matukio mbalimbali ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo joto kubwa , Baridi kali, Mvua kubwa za muda mfupi, Matukio ya Ukame, Matukio ya mafuriko ambayo yanaendelea kuongezeka kwa idadi na ukubwa wa matukio.
Hata hivyo suluhisho lake ni kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam kama vile kupanda mitikadri inavyowezekana lakini vilevile kuzingatia taarifa za mamlaka ya hali ya hewa za kila mwezi , Kila msimu na na kila siku hii itatuwezesha kuweza kupunguza athari zitokanazo na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza ufanisi na tija katika mipango yetu ya kila siku.
“Niwatake wananchi wote kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri wa hali ya hewa lakini vilevile kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira,” amesema Dkt. Chang’a
Amemtaka kila mwananchi kujiuliza swali ameifanyia nini nchi yake ya Tanzania katika kuhifadhi mazingira na kuinua uchumi wa nchi yetu.


