Baadhi ya wananchi wakitazama mfumo wa gari ambalo linatumia gesi asilia mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda akitazama mfumo wa gari unaotumia gesili asilia mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam
****************
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC limesema kuwa kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa mpaka sasa ni futi za ujazo Trilioni 57.5 kimeendelea kuwa msaada mkubwa kwa Watanzania kutokana na Matumizi yake kufikia asilimia 62 huku kiasi kikubwa kikiwa baharini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt.James Mataragio wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea Dar es salaam.
Amesema kiasi kikubwa cha gesi ambacho kipo baharini kinatarajiwa kuvunwa kupitia mtambo wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika -LNG unaotqzamiwa kujengwa nchini ambapo baadhi ya gesi itakayopatikana itasafirishwa kwenda kuuzwa kwenye masoko ya nje y na nyingine kubaki nchini kwa ajili ya soko la ndani.
Aidha Dkt.Mataragio amewaomba Watanzania kutumia fursa hiyo kwa kuanzisha kampuni zinazotumia Gesi ili waweze kunufaika zaidi pamoja na kutumia Gesi Asilia ili kuepuka uharibifu wa mazingira.
Pamoja na hayo amewataka watanzania kwa ujumla kutembelea banda lao katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam ili kupata huduma zinazotolewa na Shirika hilo.