Home Michezo KOMBE LA CANAF 2021 KUBAKI TANZANIA NI LAZIMA , NJOONI TUISHANGILIE TEMBO-...

KOMBE LA CANAF 2021 KUBAKI TANZANIA NI LAZIMA , NJOONI TUISHANGILIE TEMBO- BASHUNGWA.

0
 
Na. John Mapepele
 
Waziri mwenye dhamana ya   nchini,  Mhe. Innocent Bashungwa  ametoa wito kwa wadau wa Michezo nchini  kujitokeza kwa wingi leo Disemba 2, 2021 kuishangilia timu ya Tanzania ya soka ya wenye ulemavu (Tembo Warriors) katika  mchezo wake wa nusu fainali na  timu Liberia ili waweze kutwaa kombe la mashindano ya Bara la Afrika ya soka kwa wenye ulemavu CANAF 2021.
 
Mhe. Bashungwa ametoa wito huo leo kufuatia  timu ya Tembo Warriors jana kufuzu mashindano ya dunia  ya mchezo huo yatakayofanyika Oktoba 2022 nchini Uturuki.
 
“Tunamshukuru Mungu kazi ya kwanza ya kufuzu kwenda  kombe la dunia tumeifikia jana kwa kuwa timu ya kwanza kufuzu, kazi ya leo  tunahakikikisha tunaibamiza  Liberia, ili tufike fainali na kulibakiza kombe nchini ili kuliheshimisha taifa letu nitoe wito  kwa watu wajitokeze kuishangilia kwa wingi na kuipa hamasa timu yetu iendelee kushinda” ameeleza, Mhe. Bashungwa.
 
Aidha, amefafanua kwamba  timu ya Tembo Warriors imeandika historia ya kuwa timu ya kwanza ya soka Tanzania kabla na baada ya Uhuru kuingia kombe  la dunia.
 
Amesema  kutokana na umuhimu wa michezo hiyo aliamua kuteua Kamati maalum ya kitaifa ili kuratibu maandalizi yote ya timu ya Tembo Warriors ili ishinde iliyosimamiwa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara yake Dkt. Hassan Abbasi
 
Mikakati tuliyojiwekea kama Wizara ilikuwa kufanya maandalizi ya kimkakati , pia napenda kumshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kutuongoza  vema kwenye kipindi chote cha maandalizi haya ambapo siku mbili kabla ya mashindano kupitia Mhe. Waziri Mkuu alitoa salam na kuichangia  timu milioni 150 kwa ajili ya  maandalizi hayo.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Michezo nchini, Yusufu Omary Singo amesema  Timu nne zimefanikiwa kuingia nusu fainali  kwenye Mashindano hayo.
 
Ametaja timu zilizoingia kwenye mzunguko wa nusu fainali na makundi yatakavyocheza  leo Disemba 2, 2021 kuwa ni
(Tanzania vs Liberia) na  (Angola vs Ghana ) 
 
Michezo hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa kumi jioni
 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa wenye ulemavu Peter Sarungi amesema  timu imeendelea kuwa na morali kubwa ya kushinda mechi ya kesho kutokana na ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini.
 
Sarungi amemuahidi Mhe. Rais Samia na  wapenda Michezo wote nchini kupambana ili kutwaa kombe hilo.
Waziri Bashungwa alipokuwa akizindua mashindano ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu CANAF 2021 Novemba 2021 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.