Home Michezo JWANENG GALAXY YAPINDUA MEZA NA KUITUPA NJE SIMBA MICHUANO YA LIGI YA...

JWANENG GALAXY YAPINDUA MEZA NA KUITUPA NJE SIMBA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA UWANJA WA MKAPA

0

SIMBA SC wametupwa nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupata matokeo ya jumla ya mabao 3-3 dhidi ya Jwaneng Galaxy FC ya Botswana kwenye mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Simba SC walianza vyema na kupata bao la kuongoza kupitia Kiungo wake, Rally Bwalya kwenye dakika ya 41, wakati huo Jwaneng Galaxy FC walisawazisha bao hilo kupitia kwa Mchezaji Rudath Wendwell dakika ya 46 na 59 wakati bao la tatu likifungwa na Mchezaji Gape Mohutsiwa dakika ya 86.

Simba SC wanatupwa nje ya Michuano hiyo kwa bao la ugenini na kuruhusu mabao mengi nyumbani licha ya kupata mabao 2-0 nchini Botswana. Jwaneng Galaxy wanafuzu makundi ya Michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya matokeo hayo dhidi ya Wekundu wa Msimbazi.

Simba SC sasa inaangukia kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederations Cup) baada ya kutupwa nje kwenye raundi hiyo.