Home Michezo TAIFA STARS YAICHAPA 1-0 BENIN UGENINI NA KUONGOZA KUNDI J

TAIFA STARS YAICHAPA 1-0 BENIN UGENINI NA KUONGOZA KUNDI J

0

Timu ya Taifa Stars imefufua ndoto za kutinga hatua ya mwisho ya mtoano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Qatar mwakani baada ya kuwachapa wwenyeji Benin bao 1-0 Mchezo uliopigwa uwanja wa Stade de l’Amitie nchini Benin.

Shujaa wa Taifa Stars ni winga hatari wa klabu ya Wydad Casablanca Saimon Msuva dakika ya 6 baada ya kuachia shuti kali lililotinga moja kwa moja.

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 nyumbani, juzi Alhamisi, Stars imefanikiwa kulipa kisasi hicho cha bao moja.

Kwa ushindi huo Tanzania inafikisha pointi 7 ikilingana na Benin wenye Point 7 ila Tanzania inaongoza kundi J nafasi ya tatu inashikwa na DR Congo watakaoshuka uwanjani kucheza na vibonde  Madagascar.