Home Michezo ARSENAL YAZIDI KUPAA YAICHAPA 3-1 SPURS UWANJA WA EMIRATES

ARSENAL YAZIDI KUPAA YAICHAPA 3-1 SPURS UWANJA WA EMIRATES

0

WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumapili Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya The Gunners yamefungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 12, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 27 na Bukayo Saka dakika ya 34, wakati la Spurs lilifungwa na Son Heung-Min dakika ya 79.
Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mikel Arteta inafikisha pointi tisa na kupanda nafasi ya 10 ikilingana kila kitu na Spurs sasa baada ya wote kucheza mechi sita.