Home Mchanganyiko WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI PROFESA MAKAME MBARAWA AKAGUA UJENZI WA DARAJA...

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI PROFESA MAKAME MBARAWA AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA SALENDER

0

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professa Makame wa pili kutoka kulia  akipata maelezo ya Ujenzi wa Daraja  Jipya la Selander kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi wa Daraja hilo Mhandisi Lulu Dunia (wa pili kutoka kulia) kuhusu Ujenzi wa Daraja hilo  ambao umefikia asilimia 93 na unatarajiwa  kukamilika Desemba 2021.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-DAR ES SALAAM)

Mwonekano wa Daraja Jipya la Selander ambapo Ujenzi wake umefikia asilimia 93 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2021.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professa Makame Mbarawa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa daraja la Salender wakati Waziri huyo alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professa Makame Mbarawa akizungumza na  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila  na wakandarasi wa mradi huo wakati alipokagua  ujenzi wa daraja la Salender wakati alipotembelea kuona utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya Mainjinia kutoka  Kampuni ya GS Engineering ya Korea  ambao wanajenga mradi huo wakimsikiliza Waziri Profesa Makame Mbarawa hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao.

Msimamizi wa Ujenzi wa Daraja hilo Mhandisi Lulu Dunia kulia  akisikiliza kwa makini maagizo ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa hayupo pichani wakati akiagiza mambo mbalimbali ili kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professa Makame Mbarawa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila  na  Msimamizi wa Ujenzi wa Daraja hilo Mhandisi Lulu Dunia wakiwa katika picha ya pamoja na wahandisi mbalimbali wanaotekeleza ujenzi wa daraja la Salebder.