Home Michezo MATUKIO KATIKA PICHA TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE TANZANITE

MATUKIO KATIKA PICHA TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE TANZANITE

0

Mechi ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanawake wenye ulemavu ikiendelea kati ya timu ya Dar Queens na Tembo katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam katika  Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzanite.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbas akifuatilia mechi ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanawake wenye ulemavu kati ya timu ya Dar Queens na Tembo katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam katika  Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzanite.

Wachezaji wa mchezo wa Karate kwa wanawake toka kituo cha Shotokan Karate wakionesha mapigo tofauti tofauti katika Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzanite, lililofanyika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam leo 16 Septemba 2021.

Mchezaji wa mchezo wa Power Arts, Power Black Nyati maarufu “Jike Jeuri” akionesha uwezo wake wa kuhimili pikipiki kupita juu ya kifua chake katika Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzanite, lililofanyika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam leo 16 Septemba 2021.

Timu ya mchezo wa rede toka Jimbo la Kigambo wenye jezi nyeusi wakichuana timu ya rede toka jimbo la Temeke katika Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzanite, lililofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo 16 Septemba 2021.

Picha na WSUM – Dar es Salaam