**********************
NJOMBE
Hatmaye serikali imekubali kujenga barabara ya Itoni Lusitu ya Mkoani Njombe kwa kiwango cha lami ili kuunganisha na ya Ludewa iliyojengwa kwa kiwango cha zege ili kurahisisha shughuli za machimbo na mawasiliano ya wakazi wa Njombe na Ludewa ambayo yamekuwa yakisumbua kwa miaka mingi sasa.
Barabara hiyo yenye kipande cha kilomita 55 inatajwa kuwa mbioni kujengwa kwa kuanza kumtafuta mkandarasi ambaye huenda atafanyakazi hiyo kwa muda mfupi zaidi kutokana na jiografia ya eneo la barabara hiyo kutokuwa na milima mikali tofauti na kipnade cha Wilaya ya Ludewa.
Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo mwanyika akiwa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika Kijiji Cha Luponde amesema Barabara Hiyo Inakwenda Kumaliziwa KM 55 nyingine na kisha kuunganishwa kwenye km 50 za zege zinazounganisha miradi ya Liganga na Nchuchuma.
Nolasco Mwalongo na Denyamina Mligo ni Wakazi wa kijiji Cha Luponde ambao wamesema endapo barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami basi itasaidia sana kupunguza adha wanayoipata hasa katika kipindi cha masika.
Tayari kipande cha Wilaya ya Ludewa kimeanza kujengwa kwa zege yenye urefu wa kilomita 50 toka Lusitu hadi mawengi huku upande wa Njombe kukiendelea kuwa Kikwazo katika sekta ya usafirishaji.