Home Mchanganyiko MBUNGE MCHAFU AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU YA...

MBUNGE MCHAFU AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI MKURANGA

0

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Hawa Mchafu kupitia tiketia ya chama cha mapinduzi (CCM) wa kati kati aliyevaa kilemba cheusi akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa diwani wa kata ya Kipalang’anda  Shomari Mwambala aliyevaa kibalakashe kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Hawa Mchafu kupitia tiketia ya chama cha mapinduzi (CCM) wa kati kati aliyevaa kilemba cheusi akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa diwani wa kata ya Tengeleni Manda wa pili kushoto kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya madarasa matatu katika shule ya msingi shinikizi ya Vikangara iliyopo Wilayani Mkuranga.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Hawa Mchafu kupitia tiketia ya chama cha mapinduzi (CCM) akizungumza jambo na wananchi pamoja na viongozi wa chama baada ya halfa ya kukabidhi mifuko hiyo 100 ya saruji kwa ajili ya kusaidia kuboresha sekta ya elimu.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Hawa Mchafu kupitia tiketia ya chama cha mapinduzi (CCM) wa kulia akipata maelekezo kutoka kwa Diwani wa Tengelea mradi wa ujenzi wa Zahanati ambayo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Hawa Mchafu kupitia tiketia ya chama cha mapinduzi (CCM) akiwa mbele akiongozana na viongozi wengine mbali mbali wa chama kwa ajili ya kujionea na kutembelea eneo lenye ukumba wa hekari 8 ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji cha Magoza .

Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa wanawake (UWT) ya Chama cha mapinduzi CCM  Mkoa wa Pwani Farida Mgomi akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

……………………………………………………………..

NA VICTOR  MASANGU,MKURANGA

KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu Mbunge wa  wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) Mh. Hawa Mchafu ameamua kuchangia mifuko 100 ya sarufi katika kata mbili za Tengeleni na Kipalang’anda kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi pamoja na sekondari.

Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji katika halfa fupi  ambayo ilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama cha mapinduzi katika ngazi za kata wilaya,na Mkoa  akiwemo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani  Mbinge huyo alibainisha kwamba  ametoa mifuko 50 katika kata ya Tengeleni na mifuko mingine 50 katika kata ya Kipalang’anda ambayo itasaidia katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari sambamba na kufanya ukarabati katika shule ya msingi msingi ya vikangara ya shinikizi.

Mchafu aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais Mama Samia Suluhu ni kuendeleza zaidi kuboresha sekta ya elimu hivyo ameamua kusapoti elimu kwa lengo la kuwaondolea changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zikiwakabili wanafunzi kutembea umbari mrefu na baadhi ya kusoma katika mazingira ambayo sio rafiki.

“Kimsingi ndungu zangu nimekuja Wilayani Mkuranga na ninashukuru nimepokelewa vizuri na Mkuu wa Wilaya na lengo langu kubwa ni kuja kutekeleza ilani ya chama sambamba na ahadi zangu  nilizozitoa wakati wa kampeni kwa hiyo nimetoa mifuko hii 100 ya sarufi ambayo itagawanywa katika kata hizo mbili pamoja na kuja kuwapa mrejesho kwa kile ambacho tumekijadili katika kipindi chote cha bunge letu la bajeti la mwaka huu ili mjone jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyojipanga katika kuleta maendeleo kwa wananchi,”alisema Mchafu.

Katika hatua nyingine Mchafua aliwaahidi wananchi wa Mkurunga kuendelea kushirikiana bega kwa began a katika kusikiliza kero na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili na kwamba waendelee kumwombea  Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan katika masuala mbali mbali na kushiriki katika shughuli mbali mbali ili  kuweza kujikwamua kiuchumi.

Awali Mkuu  mpya wa Wilaya ya Mkuranga Mh.  Hadija Ally  amefarijika sana na ujio wa Mbunge huyo kwenda kufanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya yake na kuchangia mifuko 100 ya sarufi kwa lengo la kukabilian na changamoto  mbali mbali  za miundombinu zilizopo katika shule za msingi na sekondari na kwamba msaada huo utakuwa ni chachu katika kuboresha sekta ya elimu.

“Kwa kweli huyo Mbunge wetu wa viti maalumu Mkoa wa Pwani tumetoka naye mbali sana naweza kusema anajituma sana katika kutekeleza majukumu yake kwa vitendo na mimi ni mwalimu wangu mzuri sana na katika hili nimpongeze sana maana katika Mkoa wa Pwani mmepata bahati ya kupata jembe kweli kweli na mkimtumia vizuri atakuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa wananchi.”alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa wanawake (UWT) ya Chama cha mapinduzi CCM  Mkoa wa Pwani Farida Mgomi aliwaeleza wananchi kwamba lengo lao kubwa ni kuwaletea maendeleo na kwamba yale yote ambayo yanafanyika ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho na kutumia fursa hiyo kumpongeza kwa dhati Mbunge Hawa Mchafu kwa kuweza kufanikiwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo lengo ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo.

Naye Diwani wa Kata ya  Tengelea  Shabani Manda alibainisha kuwa juhudi kubwa ambazo amezifanya Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani zitaweza kusaidia na kuleta mabadiliko chnaya ya kimaendeleo na kwamba sapoti hiyo ya mifuko 50 waliyopatiwa itakwenda kufanya ukarabati katikamadarasa ambayo wanasomea wanafunzi wa shule ya msingi shikizi ya Vikangara ili wanafunzi hao wameze kusoma kaatika mazingira ambayo ni rafiki.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kipalang’anda Shomari Mwambala amempongeza Mbunge huyo kwa ktekeleza ahadi zake alizozitoa kwa wananchi kwa vitendo na kwamba mifuko hiyo ya sarufi itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuanza harakati za mradi wa ujenzi huo wa shule ya sekondari na kuwaondolea adha wanafunzi wa kutembea umbari mrefu.

Kadhalika aliongeza kuwa kwa sasa tayari wameshatenga eneo lenye ukumbwa wa hekari zipatazo nane kwa ajili ya kuanza mradi wa ujenzi huo na kwamba kutahitajika nguvu zingine za zihada kutoka serikalini pamoja na wadau wengine mbali mbali wa maendeleo ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea katika suala zima ya kuboresha elimu.

KATIKA ziara hiyo ya kikazi ya siku moja   imeweza kuzaa matunda katika kufanikisha kuboresha sekta ya elimu  imefanywa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kwenda kutekeleza ahadi zake mbali mbali alizozitoa kwa wananchi pamoja na kuwaeleza mambo mbali mbali ambayo yaliweza kujadiliwa katika kipindi chote cha bunge la bajeti  ya mwaka huu.