Home Mchanganyiko PSSSF YAENDESHA SEMINA KWA WASTAAFU DODOMA

PSSSF YAENDESHA SEMINA KWA WASTAAFU DODOMA

0

 

MTAKA: Semina za kustaafu zianze kwa Vijana

*Ashauri
Watumishi kujipanga vyema kustaafu

*Aipongeza
PSSSF kwa kuandaa semina

*PSSSF:
Semina hizi ni endelevu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Bw.
Anthony ameushauri Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
kuwashirikisha Vijana wanaoanza kazi katika mafunzo ya kujiandaa kustaafu kwani
mipango ya kustaafu huanza pale mtu anapoajiriwa.

Bw. Mtaka alitoa ushauri huo
Jijini Dodoma alipokuwa akifungua semina kwa Wastaafu wataraji wa PSSSF kwa
wananchama wa Mfuko huo mkoani Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Bw.
Anthony Mtaka akizungumza wakati akifungua semia kwa Wastaafu watarajiwa wa
PSSSF wa jijini Dodoma.

“Maandalizi ya kustaafu
yanaanzia pale mtu anapoajiriwa, hivyo ni vyema katika semina zijazo
mkawashirikisha vijana ili waweze kujipanga vyema kwa ajili ya maisha yao baada
ya ajira” alishauri Bw. Mtaka.

Mkuu huyo wa mkoa aliwashauri
wastaafu kufanya miradi watakayoimudu baada ya kustaafu na kuachana na miradi
ambayo itawaigiza katika matatizo.

“Hakikisha unachagua mapema
sehemu ambayo utaishi baada ya kustaafu, andaa vyema kitu utakachofanya,
achaneni na miradi itakayowafanya mkope na kubwa kuweni makini na matumizi
yenu”alishauri Bw.Mtaka.

Bw. Mtaka aliipongeza PSSSF
kwa kuandaa mafunzo kwa Wastaafu watarajiwa, alisema jambo hili ni zuri kwani
linawapa mwanga wa kujiandaa wastaafu watarajiwa wa Mfuko. Pia alizipongeza
taasisi mbalimbali zilizotoa elimu katika mafunzo hayo.

Akizunguza kabla ya
kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Kaimu Mkurugenzi wa PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa
alisema, jukumu la Mfuko ni 
kutoa
elimu kwa umma katika maeneo ya msingi, kama vile; Uanachama na Michango, Mafao
na mambo muhimu yakuzingatia   katika ajira, wakati wa kustaafu na baada ya
kustaafu.

Kaimu Mkurugezi Mkuu PSSSF, Bw. Mbaruku
Magawa akizumgumza katika semina kwa ajili ya Wanachama wa PSSSF mkoani Dodoma

Katika kuhakikisha wanachama wetu wanapata mafunzo ya
uhakika katika uwekezaji, tumewaalika wenzetu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogo Vidogo (SIDO) ili kuwapatia ujuzi Wastaafu wetu watarajiwa, ili waweze
kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo na hatimaye kutengeneza ajira kwa vijana
wetu” alifafanua Bw. Magawa 

Wastaafu watarajiwa wa PSSSF wakifatilia
semina waliyoandaliwa na PSSSF jijini Dodoma

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema, mpango huo wa semina ni
endelevu ambao utaendeshwa kila mwaka kwa wanachama wa PSSSF waliobakiza
kipindi kisichozidi miaka miwili kabla ya kustaafu.
Semina hiyo iliendeshwa na PSSSF kwa kushirikiana na TBP, NMB,
NBC, CRBD, DCB, SIDO, TAKUKURU, TCRA,
BENKI YA AZANIA, MCB na
UTT
AMIS.