Home Mchanganyiko PROF.MKUMBO AZINDUA BODI YA UONGOZI YA CHUO CHA CBE

PROF.MKUMBO AZINDUA BODI YA UONGOZI YA CHUO CHA CBE

0

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Dotto James akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Chuo Kikuu cha Biashara (CBE) Prof.Eliuther Mwageni akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof.Emanuel Mjema akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Chuo Kikuu cha Biashara (CBE) Prof.Eliuther Mwageni (kulia)akiapa katika uzinduzi wa Bodi ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akizindua Bodi ya Uongozi ya Chuo  cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akipata picha ya pamoja na baadhi washiriki wa uzinduzi wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam

**********************************

Waziri wa Viwanda na Biashara,Prof. Kitila Mkumbo,ameitaka Bodi ya Chuo Cha Biashara (CBE),kufanya kazi kwa weledi ili kufanikisha adhima ya Serikali ya awamu sita ya kuwaletea Maendeleo wananchi.

Prof.Mkumbo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Bodi ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

Prof. Mkumbo amesema serikali inaimani na Bodi hiyo kwa kuchagua watu wenye weledi hivyo anamatumaini watafanyakazi na kuleta manufaa kwa umma.

“Matumaini yangu Bodi itasimamia menejimenti vizuri ya Chuo hiki na kuhakikisha mnawapika wahitimu wazuri watakaokwenda kujenga uchumi wa Viwanda pamoja na  kujitengenezea ajira na kuajiri vijana”. Amesema Prof.Mkumbo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Eleuther Mwageni amesema kuwa watahakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na welede madhubuti.

Hata Hivyo,Prof. Mkumbo ameikumbusha bodi hiyo kuhakikisha wanatatua changamoto mbali mbali ikiwemo migogoro itakayojitokeza.