Home Michezo SIMBA SC YAHITAJI POINTI MOJA KUWA MABINGWA WAPYA WA LIGI BARA

SIMBA SC YAHITAJI POINTI MOJA KUWA MABINGWA WAPYA WA LIGI BARA

0

*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Simba Sc sasa yabakisha pointi moja kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu bara mara baada ya kuchapa KMC mabao 2-0 leo katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba Sc ilianza kwa kupata bao la mapema kupitia kwa mshambuliaji wao Chris Mugalu dakika ya 03 ya mchezo.

Simba iliendelea kulisakama lango la KMC kwa kuhitaji mabao zaidi licha ya kosakosa kibao kutokea.

Bao la pili la Simba Sc klabu lilifungwa tena na mashambuliaji wao Chris Mugalu mnamo dakika ya 44 ya mchezo.

Beki kisiki wa KMC, Andrew Vincent alitolewa kipindi cha pili kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.